Na Felix Mwagara, Mwanza. 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (pichani) , amefiwa na mdogo wake aitwae Josiah Chitage Lugola, aliyekua anaishi jijini Mwanza. Waziri Lugola ambaye ndiye Msemaji wa familia hiyo, alisema mdogo wake Josiah (51) alifariki dunia leo asubuhi Oktoba 7, 2018 na mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika Hospitali ya Sekour Toure, jijini Mwanza. 
Waziri Lugola aliongeza kuwa, msiba upo Kijiji cha Nyamitwebili, Kata ya Nyamihyolo, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda Mkoa wa Mara. Waziri Lugola alikua wilayani Bunda kikazi ndipo akapata taarifa hizo za kushtukiza za msiba wa mdogo wake. 
Waziri Lugola alisema msiba huo ni wa ghafla, umeshtua familia na hakika mdogo wake huyo ameacha pengo kubwa katika ukoo wao. 
"Msiba huu ni mkubwa, na pia umetikisa familia yetu, kifo kinapangwa na Mungu, hivyo tunamuombea Mungu, mdogo wangu apokelewe peponi, amina," alisema Waziri Lugola. 
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, ametoa pole kwa Waziri Lugola pamoja na familia kwa ujumla. 
"Wizara inatoa pole kwa familia ya Waziri Lugola, ndugu wote, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo," alisema Kingu.
 Kwa mujibu wa msemaji wa familia hiyo, taarifa za mazishi zitatolewa baada ya kikao cha familia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...