Waziri wa Maji, Profesa Makame ameziagiza Halmashauri zote kufanya utafiti wa kina kwa wakandarasi kabla ya kuingia nao mikataba ya ujenzi wa miradi ili kuweza kumaliza tatizo la utekelezaji mbovu wa miradi ya maji nchini.

Amesema tatizo la miradi mingi ya maji kwenye halmashauri ni kwa sababu zabuni nyingi zinatolewa kwa wakandarasi wasio na sifa, wengine wakishindwa hata na miradi midogo wakati akikagua miradi ya maji ya Kumbara-Litola, Milonje-Matemanga na Milonde katika Wilaya za Namtumbo na Tunduru, mkoani Ruvuma.

Profesa Mbarawa amesema halmashauri nyingi zimekuwa zikitoa zabuni kwa wakandarasi katika mazingira ya rushwa, bila kuzingatia uwezo wao kifedha, vifaa vya kazi na kazi zao kwa sababu hawafanyi uchunguzi wa kina hivyo kusababisha matatizo kwenye utekelezaji wa miradi. Jambo linalosababisha kubadili wakandarasi mara kwa mara kutokana kuvunja mikataba mara mara kwa sababu ya utendaji mbovu wa wakandarasi, na kurudisha nyuma juhudi za Serikali kuwapatia wananchi wake huduma ya majisafi na salama.

"Serikali haitakubali kurudishwa nyuma kimaendeleo na mtu yeyote, tutawafukuza wakandarasi wasio na sifa na tutashughulika na wale wote wanaotoa zabuni pasipo kufuata utaratibu lazima niwaambie ukweli'', amesema Profesa Mbarawa.

"Ni lazima mfanye uchunguzi wa kina kwa kila mkandarasi kwa kuzingatia vigezo vyote, ikiwa ni pamoja na kwenda kuangalia kazi walizozifanya kwa lengo la kujiridhisha uwezo wake kabla hamjaingia nao mkataba'', ameonya Profesa Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa ameagiza Kampuni ya Service Plan Ltd isipewe tena kazi na wizara yake, baada ya kubainika imetoa taarifa ya usanifu wa mradi wa Kumbara-Litola isiyo sahahi uliopo Wilaya ya Namtumbo ambapo ungeigharimu Serikali fedha nyingi bila sababu.

Kulingana na usanifu wa awali kuonyesha gharama kubwa, ililazmika kufanya usanifu upya na kuonekana unaweza kutekelezwa kwa Shilingi Bilioni 1.2 baadala ya Shilingi Bilioni 6 kama ilivyoonyesha awali na mradi huo unategemewa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Sophia Kizigo (kulia) na wataalamu katika chanzo cha mradi wa Milonde, Namtumbo, mkoani Ruvuma.
Mradi wa maji Milonde ukiwa katika hatua ya utekelezaji.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akikagua tenki la mradi wa Kumbara-Litola, Namtumbo na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Sophia Kizigo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...