* Ifikapo Jumatano awe amepeleka walimu shule ya msingi Rwenzige
*Ina wanafunzi 216 wa darasa la awali hadi la nne bila mwalimu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku mbili kwa Kaimu Afisa Elimu (Msingi) wa wilaya ya Muleba, mkoani Kagera Bw. Bukuru Malembo awe amepeleka walimu wawili katika shule ya msingi iliyoko kwenye kitongoji cha Rwenzige kwa kuwa haina mwalimu hata mmoja.

Shule hiyo yenye madarasa wawili na ofisi moja ya mwalimu ina jumla wanafunzi 216 wa darasa la awali hadi la nne, ilijengwa na wananchi ambapo wanafunzi wake wanafundishwa na mwananchi mmoja aliyemua kujitolea ili kuwapunguzia watoto kutembea umbali wa kilomita 16 kwenda kusoma katika shule ya kijiji cha Kiteme.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumatatu, Oktoba 8, 2018) baada ya wanafunzi wa shule hiyo kuwasilisha malalamiko yao kwa njia ya bango wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha kituo cha afya Kimeya, baada ya kukagua majengo ya kituo hicho.

“Haiwezekani watoto wadogo wenye umri wa kuanzia miaka mitano wakatembea umbali wa kilomita 16 kwenda shule wakati katika kitongoji chao kuna shule yenye madarasa mawili na chumba kimoja cha ofisi ya mwalimu na Afisa Elimu hadi sasa hajapeleka walimu na kumuachia mwalimu Benson (kijana ambaye si mwalimu ila anajitolea kufundisha) akifundisha wanafunzi hao peke yake.”


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa wilaya ya Muleba, DKt. Modest Buchari (kulia) wakati walipokagau ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba (kulia), Oktoba 8, 2018.Wanne kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti.

aziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakimjulia hali, Consolata Marios na mwanae Revina Albert wakati walipotembelea wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakizungumza na Bibi Saura Venant na aliyempakata mwanae, Anord Revocatus (kushoto) na Bibi Dorothea Fidel aliyempakata mwanane Redemta Deobey (wapiki kushoto) wakati awalipotembelea wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018.

Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018

Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa na Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa AnnaTibaijuka (mwenye gauni la bluu) wakicheza ngoma ya asili wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba kuhutubia mkutano wa hadhara, Oktoba 8, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...