ZAIDI ya kaya 200 katika mtaa wa Mnyanjani kata ya Myanjani Jijini Tanga zitanufaika na mradi wa ujenzi wa mtaro kwa ajili ya kuondoa tatizo la mafuriko linalotokea kila nyakati za msimu wa mvua. 

Hayo yamebainishwa na Mhandisi toka Wakala wa Usimamizi wa barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoani Tanga Omari Saidi wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya jitihada za kuzinusuru kata hizo. 

Mhandisi Saidi alisema mradi huo unaokadiriwa kutumia Shilingi Milioni 170 umeelekezwa katika eneo hilo lililokuwa na hali ya kutuama kwa maji kila mwaka nyakati zote za mvua na kusababisha mafuriko na kupelekea wananchi kulazimika kuyahama makazi yao. Alisema mradi wa mtaro huo ambao utakuwa na urefu wa mita 512 utakuwa na uwezo wa kusukuma maji kuelekea bahari na kuzifanya kaya hizo na maeneo ya pembezono mwa mtaa huo kuishi kwa amani hasa nyakati za mvua. 

“Ni kweli hali ya mtaa huu haikua ya kuridhisha sisi tarura ambao tunamamlaka sasa tumeona hiki ndio kipindi cha kurekebisha miundombinu ya mifereji namea mvua zitakapo nyesha kaya hizi zitakuwa sehemu salama”Alisema Saidi. Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF) Alhaj Mussa Mbaruku ambae alitembelea mradi huo jana alisema matumaini makubwa yanaonekana ya kuwanusuru wananchi hao na mafuriko yanayotokea kila mwaka.

 Alhaj Mbaruku alisema eneo hilo limekuwa kero kwa wananchi hao ambao kila nyakati za mvua maisha yao yanakuwa hatarini kutokana na hofu ya mafuriko yanayosababishwa na mvua za misimu na kulazimika kutafuta makzi mapya. 

“Taratibu hali ya maeneo yaliyokuwa yanakumbwa na mafuriko ndani ya Jiji yanaanza kuwa na hali nzuri baada ya taasisi hiyo kuwa makini na utekelezaji wa ujenzi wa mifereji hasa katika maeneo yanayotuama maji”Alisema Alhaj Mbaruku. Hata hivyo aliiomba taasisi hiyo kuendeleza kasi yao na mbali ya miradi ya mifereji pia ihakikishe kuwa barabara zote ndani ya Jiji hili zinaweza kutumika nyakati zote na zinajengwa kwa kiwango cha lami huku akiongeza kusema kuwa ulazima wa uwepo wa barabara za lami ndani ya jiji lazima uzingatiwe. 

Awali akizungumzia kero hiyo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Bakari Haule alisema tatizo la mafuriko katika eneo hilo lililkua ni kubwa mbali ya nyumba hizo kujengwa katika mpangilio lakini adha kubwa ilikuwa ni kutuama kwa maji nyakati za mvua.
 MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea mradi wa Ujenzi wa Mradi wa Mfereji utakaopitisha maji kutoka kwenye makazi ya watu nyakati za mvua na kupelekea baharini 
 MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro eneo la Mnyanjani Jijini Tanga ambao utasaidia kuondoa kero ya kutuama maji kwenye makazi ya wananchi wakati wa mvua wakati alipofanya ziara ya kuutembelea
Mtaro utakaopitisha maji kwenye eneo la Mtaa wa Mnyanjani Jijini Tanga ya mvua na kupelekea baharini ili kuwaepusha wananchi na mafuriko nyakati za mvua
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia aakimuonyesha kitu Mhandisi toka Wakala wa Usimamizi wa barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoani Tanga Omari Saidi wakati alipotembelea ujenzi wa mradi wa Mtaro 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...