Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii



Msanii wa muziki wa Bonofleva Ali Kiba amemjibu msanii mwenzake Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz'  kuptia ukurasa wake wa Instagram kuwa amekubali mualiko wa kwenda kushiriki katika tamasha la Wasafi Festival.


Katika ujumbe wake Ali Kiba amesema kuwa, ameshukuru kwa kupata mualiko wao ila hataweza kushiriki kutokana na kuwa na majukumu mengine ya kuzindua kinywaji chake cha Mofaya Energy.

Mbali na hilo Kiba amemuomba Diamond kudhamini tamasha hilo ili kusongesha gurudumu la muziki wa Tanzania.

"Pia ndugu zangu #Wasafi tumepata "Salamu zenu (Wasafi) nimepata. Nashukuru kwa mualiko wenu, ila kwa bahati mbaya sitoweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi zingine. Hata hivyo tusingependa kuwaacha hivi hivi, tupo tayari kuwapa support ya kudhamini tamasha lenu kupitia #MofayaEnergyDrink ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Africa . Management #RockstarAfrica yangu tutaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya hili jambo kubwa "

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...