Na Mwandishi wetu
Benki ya TPB imeendelea kuisadia  klabu ya  Waandishi wa habari za michezo  nchini (Taswa SC) baada ya kuikabidhi vifaa vya michezo ambavyo vitatumiwa na timu hiyo katika michezo yake mbalimbali.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja  Mawasiliano wa  Benki ya TPB Chichi Banda alisema kuwa wamesaidia msaada huo ni sehemu ya shughuli za Benki na kutambua mchango mkubwa wa Waandishi wa Habari Nchini na muendelezo wao katika shughuli za kijamii ambapo mbali ya michezo, pia usaidia afya na elimu.

Chichi alisema kuwa wamefariji kakutoa msaada huo kwaTaswa SC ambayo mara kadhaa imekuwa ikitwaa ubingwa katika mashindano maalum ya vyombo vya habari yanayofanyika kila mwaka mkoani Arusha.

Alisema kuwa benki ya TPB ni wadau wakubwa wa michezo na mbali ya Taswa SC, pia usaidia timu nyingine.

“Waandishi wa habari wameonyesha mfano mkubwa kwa kucheza soka na netiboli, wameamua kuhamasisha michezo katika jamii, kwa vitendo, hii imetupa faraja kubwa sana kwetu, ”alisema Chichi.

Mwenyekiti waTaswa SC, Majuto Omary aliishukuru benki ya TPB kwa kuendelea kuwakumbuka na kuahidi kutumia vifaa hivyo  kwa umakini mkubwa na kushinda katika mechi zao mbalimbali.

“Tunajivunia uwepo wa Benki ya  TPB kwa kuthibitisha kuwa ni benki halisi ya Watanzania, nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania kufungua akaunti zao katika benki hii na vile vilekuomba wadau wengine kufuata  mfano  kwa kuisaidiaTaswa SC ili iweze kufanikisha shughuli zake,” alisema Majuto.
 Meneja Mawasiliano wa TPB Bank, Chichi Banda (Kulia) akikabidhi jezi kwa Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari za Michezo Nchini (Taswa SC), Majuto Omary katika hafla fupi iliyofanyika jana. TPB Bank imetoa msaada ikiwa sehemu ya shughuli zao za kijamii.
Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari za Michezo Nchini (Taswa SC), Majuto Omary (kulia) akitoa neon la shukrani mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na Meneja Mawasiliano wa TPB Bank, Chichi Banda katika hafla fupi iliyofanyika jana. TPB Bank imetoa msaada ikiwa sehemu ya shughuli zao za kijamii. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...