Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Veronika Kesi ametoa amri ya kupewa adhabu  ya kuchapwa viboko kwa vijana au mtu yeyote atakaye onekana kuvaa mavazi yasiyo na staha katika jamii ya wakazi wa Makete.
  
Mkuu wa wilaya ametoa agizo hilo alipo kuwa katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi wa kata za Iniho na Kipagalo ambapo amesema mavazi hayo sio maadili ya wakazi wa wilaya yake  pamoja na Tanzania kwa Ujumla.

Bila kueleza idadi gani ya viboko itolewe kwa vijana wakiume wanaovaa suruali mlegezo (chini ya makalio) au wasichana kuvaa mavazi yanayobana au yanayoonesha maumbile yao au mavazi yanayochora miili yao wachapwe viboko tangu kutolewa kwa amri hiyo wakati akizungumza na wakazi wa kata hizo.

''Nataka kuona vijana suruali zenu zinashuka kutokana na wallet kuwa nzito umefanya shughuli zako huko walleti imejaa hela ndio ina inashusha sio kushusha tu ni viboko nasisitiza ni viboko wakati sheria za adhabu zingine zikiendelea kutungwa huko kwenye kata''

Amesema kuwa kuanzia sasa viboko vianze kuchapwa kwa kila mtu atakaye vaa hivyo na kumtaka mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Makete  Godfrey Gogadi kushirikiana na serikali za vijiji kutunga sheria itakayomhukumu na kupewa adhabu kwa watu wa aina hiyo.

''huu ni utamaduni wa wapi?? sie wabantu hatuna utamaduni huo naagiza mkimkamata chapa viboko tu,watoto wetu hao!''

Kwa upande wake wake Mwanasheria bw Godfrey Gogadi amesema ameshaanza kuwasiliana na viongozi wa serikali ili kuanza kutunga sheria ndogondogo za kusimamia agizo hilo.

''Tumeanza kukusanya maoni ya Wadau kwa watendaji ili kutunga sheria hizo ndogodndogo kama mkuu alivyosema ila wakati hilo likiendelea viboko viendelee maana anavyo vaa chini ya makalio anakwambia anataka viboko hivyo nikupiga Tu''

Aidha Mkuu huyo wa wilaya akiendelea kusikiliza kero za wananchi amesistiza kuwalea watoto katika maadili na kuwalinda dhidi ya ukatili ikiwemo ubakaji na mimba za utotoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...