Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
Serikali imesema ndani ya miaka mitatu inatarajia kujenga vituo vya afya 67 katika maeneo mbalimbali nchini. 

Aidha imesema ndani ya kipindi hicho upatikanaji wa  dawa kwa wastani kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya afya na hospitali nchini umefikia asilimia 90.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan Abbas, amesema hayo leo Novemba 3.2018 alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) yaliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Akizungumza katika mafunzo hayo, Dk. Abbas amesema serikali imeahidi kuboresha huduma ya afya mijini na vijinini kwani tangu kupata Uhuru imejenga Hospitali 77 na sasa inaenda kujenga vituo 67 na kuhakikisha azma ya kutekeleza Huduma ya afya inatekekezwa.

Akizungumzia upatikanaji wa dawa, Dk. Abbas amesema miaka ya nyuma upatikanaji wa dawa kwa zahanati, vituo vya afya na hospitali ilikuwa shida hasa kutokana na mfumo uliokuwa unatumika kusambaza lakini kwa sasa jambo ambalo sasa jambo hilo limedhibitiwa.

Amesema, Serikali ya Awamu ya Tano imetenga bajeti ya kutosha hali MSD kuweza kuagiza na kusambaza dawa kwa wakati.

"Kwa sasa Tanzania imekuwa kimbilio la nchi zingine kwa kuleta wagonjwa wao kutokana na uwepo wa vifaa tiba na wataalam katika hospitali mbalimbali nchini ambao wanatoa mpaka tiba za kibingwa", amesema Dk. Abbas.

Ameongeza kuwa, Tanzania sasa imeanza  kuwa kimbilio kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa katika hospitali zetu, sasa hivi wanapokelewa wagonjwa kutoka Comorro,  Burundi, Rwanda,  Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na nchi zingine wanakuja Muhimbili kuja kutibiwa.
 Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan Abbas  akizungumza na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) kuhusiana na mafunzo ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) yalifanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF Mbaruku Magawa akizungumza na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) kuhusiana na bidhaa zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)katika mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mtendaji wa DCPC  Hussein Siyovelwa akizungumza kuhusiana umuhimu wa wanachama kufanya kazi kwa ukaribu na NHIF katika utoaji wa taarifa kwa jamii .
 Meneja wa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Angela Mziray akitoa maelezo  kwa wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC)  kuhusiana na utoaji wa elimu katika makundi mbalimbali  ya  katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) yalifanyika jijini Dar es Salaam.
Picha za pamoja za makundi mbalimbali  katika mafunzo( Picha na  Chalila Kibuda, Globu ya Jamii)

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...