Na Rhoda James- Morogoro
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewaeleza wahasibu wa madini nchini kuwa wizara haitamvumilia mtu yeyote ambaye atakuwa chanzo cha upotevu wa ukusanyaji wa mapato ya Serekali. Nyongo ameyasema hayo wakati akifunga Mafunzo ya Kielektroniki ya Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali ambayo yaliaanza tarehe 12 hadi 15 Novemba, 2018 katika Chuo cha Mazimbu Campus kilichopo mkoani Morogoro.

Naibu Waziri Nyongo amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza tija na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato  serikalini.  Akizungumza katika Kikao hicho Nyongo alisema kuwa Viongozi wote wako tayari kutoa msaada wowote masaa 24 hivyo kama kuna mhasibu ambaye atakuwa na uhitaji kwa masuala ya kikazi asisite kuwasiliana nao waati wowote. 

Aidha, Nyongo alieleza kuwa tasnia ya uhasibu ni ya muhimu sana katika sekta ya madini, hivyo ni vyema kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa katika malengo yake akahakikisha kuwa anafikiria lengo la ndani la Wizara la ukusanyaji wa Bilioni 500 linatimizwa. Pamoja na hayo, Nyongo alitoa pongezi kwa wahasibu wote kwa kufanikisha kufikia lengo la wizara katika ukusanyaji wa mapato ya kiasi cha tsh Bilioni 310 kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 na kuwataka jitihada iliyotumika itumike katika kufanikisha lengo la muhula huu wa fedha.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akihutubia Wahasibu (hawapo pichani) wakati wakiwa katika mafunzo ya Kielektroniki ya Ukusanyaji Mapato ya Serikali mkoani Morogoro.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uhasibu, Anthony Tarimo akihutubia Wahasibu (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya Kielektroniki ya Ukusanyaji wa Mapato ya Serikalini mkoani Morogoro.
Wahasibu mbalimbali kutoka Wizara ya Madini pamoja na Wahasibu kutoka Tume ya Madini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) wakati wa Mafunzo ya Kielektroniki ya Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati kwa waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na waiohudhuria mafunzo hayo mara baada ya kufunga mafunzo ya Kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali mkoani Morogoro.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...