WAJUMBE wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar imekiri kujifunza mambo makubwa katika ujenzi wa jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB3), imeelezwa.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambayo ilikuwa na ziara kwenye jengo hilo na Mhe. Mohammed Said (Mwakilishi wa Mpendae), amesema ujenzi wa jengo hilo ni fundisho tosha kutokana na kwenda kwa kasi tangu ujenzi wake uanze Juni 2013, tofauti na ujenzi wa jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Amani Abeid Karume umechukua takribani miaka 10 tangu mwaka 2009 lakini hadi sasa lina asilimia 39 pekee.

Mhe. Said amesema TB3 ni jengo la kisasa kutokana na miundombinu yake ambayo mingi inaendeshwa kwa mifumo maalum, ikiwemo sehemu ya mizigo, ambayo inaendeshwa kupitia hatua tano.

“Katika ziara hii tumefarijika sana kwani tumejifunza mengi wenzetu walivyoweza kuufikisha mradi huu, kwa kweli tumechukua yote na tutakwenda kuishauri serikali namna bora ya kuendeleza ujenzi wa majengo na viwanja vya ndege kwa ujumla,” amesema Mhe. Said.

Hali kadhalika, Mhe Said amesema mbali na kutembelea jengo hilo, pia wamepata maelezo mazuri ya kiutendaji katika uendeshaji, ukusanyaji na mgawanyo wa mapato kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), na wataishauri serikali namna bora ya kudhibiti mapato.

Mhandisi Barton Komba wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), (aliyesimama mbele), leo akitoa maelezo ya maendeleo ya mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kwa Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipofanya ziara ya mafunzo. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Lawrence Thobias (kulia mbele waliosimama), akiielezea Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar namna ya uendeshaji, ukusanyaji na mgawanyo wa mapato kwa mujibu wa sheria, wakati ilipotembelea Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. 
Mhandisi Barton Komba wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), (aliyenyoosha mkono) akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar leo ilipotembelea Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...