Na Lucas Mboje, Iringa;
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza Magereza nchini, Phaustine Kasike ametoa rai kuwa ili kupunguza msongamano magerezani ni vema jamii ikaacha kufanya matukio mbalimbali ya uhalifu hapa nchini.
Rai hiyo imetolewa leo na Kamishna Jenerali Kasike wakati akitoa ufafanuzi mbele ya wanahabari wa Mkoani Iringa kuhusu madai ya uwepo wa msongamano wa wafungwa katika magereza mbalimbali yaliyopo nchini ambapo ameeleza kuwa si kweli kwamba magereza yote yana msongamano bali msongamano uliopo magerezani ni kwenye baadhi ya magereza yenye kuhifadhi mahabusu.
Amesema suala la msongamano limekuwa ni tatizo kubwa ambapo takwimu za Jeshi la Magereza zinaonesha kuwa idadi ya mahabusu waliopo magerezani ni wengi na hali hiyo inatokana na wingi wa matukio ya uhalifu kwenye eneo husika na kule ambako hakuna uhalifu mwingi basi nako kwenye magereza hakuna msongamano mkubwa wa wafungwa/mahabusu.
Ameongeza kuwa Jeshi la Magereza litaendelea kushirikiana na vyombo vya haki jinai ikiwemo Jeshi la Polisi, Mahakama na Ofisi ya DPP ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na usukumaji wa kesi mbalimbali za mahabusu waliopo magerezani.
“Tutajitahidi kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika jukwaa letu la haki jinai ili kuangalia namna bora zaidi ya kuweza kutatua tatizo la ucheleweshaji wa kesi za mahabusu waliopo magerezani”. Amesema Jenerali Kasike.
Kuhusu uhamisho wa Gereza Iringa kwenda eneo la la Mlolo, Kamishna Jenerali Kasike amesema tayari Jeshi hilo limekwishaanza kutekeleza maelekezo ya Serikali ambapo hivi sasa lipo katika mchakato wa kuhamishwa kadri hali ya kibajeti itakavyoruhusu. 
“Tumekwishaanza ufyatuaji wa tofali za ujenzi wa nyumba za maafisa na askari sambamba na ujenzi wa mabweni ya wafungwa unaendelea katika eneo hilo hivyo Gereza Iringa litahamishiwa katika eneo la Mlolo ili kupisha huduma za kijamii”. Amesisitiza Jenerali Kasike.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, CGP. Phaustine Kasike yupo mkoani Iringa  kwa ziara ya kikazi ambapo leo ametembelea magereza ya Iringa na Pawaga. Ziara hizi ni mwendelezo wa ziara zake  za kikazi zenye lengo la kukagua magereza yote Tanzania Bara na kuzungumza na Maafisa na askari pamoja na kujua changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wakitekeleza majukumu yao.

 . Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiwasili katika Gereza la Iringa leo Novemba 9, 2018 tayari kwa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua shughuli mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akizungumza na Mahabusu na Wafungwa wa Gereza Iringa(hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi leo Novemba 9, 2018.

 Askari wa vyeo mbalimbali wa Gereza Pawaga wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza alipotembelea gereza hilo leo Novemba 9, 2018.

 Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Hassard Mkwanda akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike kutembelea maeneo mbalimbali ya Gereza la Wilaya Iringa.


 6 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akikagua maandalizi ya shamba ya kilimo cha mpunga katika eneo la Gereza la Pawaga Mkoani Iringa. Gereza Pawaga limepewa malengo ya kulima ekari 375 za mpunga ili kuwezesha mpango wa kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akikagua moja la ghala la kuhifadhia mpunga unaozalishwa katika Gereza la Kilimo Pawaga(Picha na Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...