Wanariadha kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi wamejitokeza kwa wingi kushiriki Namtumbo Marathon inayotarajiwa kutimua vumbi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma ambapo maelfu ya wakazi wa wilaya hiyo na vitongoji vyake wamekuwa wakizitazamia mbio hizo kuanza wakati wowote ili nao wapate fursa mbalimbali za kushiriki katika mbio hizo.

Akizungumzia usajili unaoendelea katika hospitali ya wilaya ya Namtumbo, Dokta Chihoma amesema watu wengi wameitikia wito na wamejitokeza kwa wingi wao kujiandikisha tayari kwaajili ya kushriki mbio hizo ambazo zilianzishwa rasmi mwaka 2017 kwa malengo mengi lakini kubwa likiwa ni kuchangisha fedha kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo ambayo imefanikia kuanza kwa kiasi kikubwa. 

Aidha Chihoma ameongeza kuwa nafasi bado zipo wazi kwaajili washiriki watakaojitokeza kujiandika kwaajili ya bio hizo. 

Kwa upande wao wadhamini wa na waandaaji wa mbio hizo Mantra Tanzania au Uranium one wamesema kila kitu kipo sawasawa na kuwataka watanzania na wageni kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo ambazo zinalenga kuleta maendeleo ya kiafya katika eneo la Namtumbo na vitongoji vyake. 

Mwakilishi wa Mantra Tanzania Bi. Khadija Pallangyo Kawawa amaesema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba watanzania watafurahia mbio za mwaka huu kutokana na jinsi zilivyopata hamasa kubwa katika maeneo mbalimbali “Nawaomba sana watanzania wajitokeze kwa wingi waje washiriki nasi katika kufanikisha awamu ya pili ya Namtumbo Marathon” 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...