Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hakuna Maendeleo pasipo Utawala bora.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mwanga mkoani Kilimanjaro.

“Viongozi wa Halmashauri, Viongozi wa Wilaya wasipokuwa na Utawala bora, wasiposhirikiana, Chama, Serikali, Wilaya, Halmashauri tusitegemee kuwa na maendeleo tutalalamika siku zote” alisema Makamu wa Rais. Leo katika ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo Makamu wa Rais alitembelea miradi mbali mbali katika Wilaya ya Same na Mwanga.

Akiwa Wilayani Same, Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya New Dawn, Shule ambayo itakuwa ya mchepuo wa masomo ya sayansi na ni maalum kwa Watoto wenye mahitaji maalum na Yatima pamoja na kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ofisi za Wakala wa Misitu Wilaya ya Same.

Makamu wa Rais amewahimiza Wakala wa Misitu nchi kuwapa wananchi miche ya kutosha na kuimarisha ulinzi katika hifadhi ya misitu. Akiwa Wilayani Mwanga, Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe ambao awamu ya kwanza imekamilika kwa asilimia 76%.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe,pichani kulia ni 
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Clelia Felician wa kampuni ya M.A Kharafi & Sons wakati alipotembelea mradi mkubwa wa maji wa Same –  Mwanga – Korogwe ambao awamu ya kwanza imekamilika kwa asilimia 76%. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Sehemu ya Miundombinu ya Mradi wa Maji Same-Mwanga-Korogwe ambao asilimia 76% imekamilika. wanga-Korogwe ambao asilimia 76% imekamilika. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya (katikati) muda mfupi kabla ya mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Mwanga kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira . Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Kilimanjaro. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...