Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii Mikumi

Serikali imejenga mazingira kwa vijana kupitia mapinduzi ya viwanda kwa serikali ya awamu ya Tano chini Rais Dkt John Pombe Magufuli ambapo ndio suluhisho ya vijana wenye ujuzi kutumika katika viwanda hivyo.

Hayo aliyasema Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi katika mahafali ya 21 ya Chuo VETA Mikumi ,amesema kuwa mafunzo ya VETA ndio uwanja mpana katika soko la ajira kwa vijana kujiajiri au kuajiriwa.

Amesema vijana waliohitimu ni zaidi 315 ambapo wanaenda katika soko la ajira hivyo wanaweza kujiunga katika vikundi na kuanza kuzalisha kile walichokipata kwa miaka waliosoma chuoni hapo. Wanachuo 315 wamehitimu mafunzo kwa ngazi ya (Level) II na III, kati yao wavulana walikuwa 209 na wasichana 106.

Amesema vijana hao wanahitaji mazoezi ya kutosha ili kuweza kupambana na soko la ufundi katika Jumuia ya Afrika Mashariki hivyo ili waweze kuwa na vigezo hivyo walimu wanahitaji kuongeza nguvu za ziada kwa vijana hao hasa walioko bado katika masomo. Mgoyi aliwaasa vijana kutokuitegemea sana serikali katika kuwatafutia ajira na badala yake watumie fursa ya mafunzo walio pata VETA Kwenda kutengeneza kampuni na kujiajiri wenyewe na kuajiri wenzao.

Aliwaasa vijana kutokuwa waoga katika katika kazi zao kwa yale walio fundishwa na kuwa wajasili ili waweze kuwaambia wateje na kuwaaminisha wateja ya kuwa wao ni bora, kwani wateja hawawezi kuwaamini kama wao watashindwa kuwaaminisha. Mkuu wa Wilaya huyo ameiomba VETA kuchangamkia fursa za uzalishaji mali kama wanavyofanya Jeshi ni katika ujenzi wa uchumi wa viwanda .

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adm Mgoyi akipata maelezo kwa mwafunzi wa Kozi ya Uselemala Chuo cha VETA Mikumi Mariam Anderson wakati wa mahafali ya 21 ya Chuo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi akizungumza katika mahafali ya 21 ya Chuo cha VETA Mikumi yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho.
Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki wa VETA Geofrey Sabuni akizungumza kuhusiana na mikakati ya VETA katika utoaji ujuzi kwa vijana katika kmahafali ya 21 ya Chuo cha VETA Mikumi yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho.
Aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi Christopher Ayo akitoa salam kwa wahitimu ambao alikuwa nao wakati akihudumu cheo hicho katika chuo  katika mahafali ya 21 ya Chuo cha VETA Mikumi yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi Emmanuel Munuo akitoa taarifa ya chuo katika mahafali ya 21 ya Chuo cha VETA Mikumi yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho.
Mchoro wa Ramani waliochora wanafunzi wa kozi ya ujenzi katika Chuo cha VETA Mikumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...