Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Katika mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli makusanyo ya maduhuli ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa mwaka 2014/15 yameongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 2.9 na kufikia 10.5 kwa mwezi kwa mwaka 2018.


Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Habari maelezo leo Jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa Kwa hivi sasa makusanyo yameongezeka hadi kufikia Shilingi bilioni 10.5 kwa mwezi kwa mwaka huu 2018 huku lengo letu na mikakati ni kufikia makusanyo ya Shilingi bilioni 12 kwa mwezi.

Mhandisi Luhemeja amesema, kwa upande wa ukusanyaji wa mapato haya yanatokana na mauzo ya huduma za maji na majitaka katika eneo la DAWASA, ambalo ni jiji la Dar es salaam na miji ya Kibaha na Bagamoyo

Ameeleza kuwa, mpaka sasa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano, miradi mikubwa iliyokamilika ni pamoja na upanuzi wa mtambo wa Ruvu juu, ujenzi wa tenki la Kibamba na ulazaji wa mabomba makuu ya kusafirisha maji.

Mhandisi Luhemeja amesema, kufuatia kukamilika kwa miradi mbalimbali , maji yanayozalishwa yameongezeka na kufikia lita milioni 502 kwa siku wakati mahitaji ya maji kwa siku ni lita milioni 554, na Serikali imejipanga kumaliza tatizo la Maji Dar es Salaam ifikapo mwaka 2020 kwa upatikanaji wa huduma za maji katika jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani kufikia asilimia 95 kwa maji safi na asilimia 30 kwa maji taka.

Amesema, Katika miaka hii mitatu ya Serikali ya awamu ya tano miradi mingine inayotekelezwa ni pamoja na ile ya kufikisha huduma katika maeneo ambayo hapo awali yalikuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa kutumia fedha za ndani.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumzia mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ikiwemo makusanyo ya maduhuli kwa mwaka 2014/15 yameongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 2.9 na kufikia bilion 10.5 kwa mwezi kwa mwaka 2018 leo Jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Tanzania Dr. Hassan Abbas akimkabidhi kitabu cha nchi yetu kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja leo Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...