Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MAMLAKA ya vitambulisho vya taifa (NIDA) imeendelea kuwahimiza wananchi kujiandikisha ili waweze kupata vitambulisho vya utaifa ambavyo umuhimu na matumizi yake kwa sasa yamekuwa makubwa zaidi.

Akizungumza na blogu ya jamii Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya mamlaka hiyo Rose Joseph amesema kuwa wanataraji  kufikia malengo ya wananchi wanaosajiliwa kukidhi vigezo vya uraia (Watanzania) na wanakidhi vigezo vingine  hasa sehemu zao za makazi.

Amesema kuwa umuhimu za zoezi la mapingamizi na uhakiki wao kama mamlaka hawawezi kuwajua Watanzania wote hivyo Watanzania lazima wawe wazalendo kwa taifa letu kwani wakiruhusu wageni kujiandikisha watawapa fursa ya kumiliki ardhi na kuleta athari nyingine kama hizo.

Aidha amesema kuwa mamlaka hiyo kwa mkoa wa Dar es salaam bado wanaendelea kutoa vitambulisho kwa wananchi waliojisajili muda mrefu hivyo wananchi wafuate vitambulisho vyao katika ofisi za kata walizojiandikisha  na kuvihifadhi vizuri.

Akieleza umuhimu wa vitambulisho hivyo, Joseph amesema kuwa kitambulisho cha utaifa ndicho kinachotoa hadhi ya kutambulisha uraia hivyo amewataka wananchi kwenda katika halmashauri za Wilaya zao ambako huduma hizo zimezogezwa ili waweze kujipatia vitambulisho hivyo.

Na kwa wageni wanaokaa zaidi ya miezi sita nchini, Joseph amesema kuwa  lazima wasajiliwe na kupata vitambulisho vya utaifa kutoka mamlaka hiyo ambavyo  vitawatambulisha katika kipindi chote watakachokuwa nchini.

Pia ametoa rai kwa watanzania kutumia nafasi hiyo kwani matumizi ya vitambulisho yamezidi kuwa  makubwa zaidi hivyo ni vyema kila mtanzania mwenye vigezo akawa navyo.
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa (NIDA) Rose  Joseph  akizungumza na Michuzi Blog kuhusu watanzania kuendelea kujisajili katika ofisi za NIDA zilizopo katika ofisi za wakuu wa Wilaya nchi nzima.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano NIDA, Rose Joseph (kushoto) akiteta jambo na  Mkuu wa Kitengo cha Vihatarishi jambo,Steven Kapesa. (picha na Emmanuel Massaka MMG.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...