Na: Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma.

Serikali imeendelea kuchukua hatua za kubatilisha milki za ardhi za mashamba yaliyotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamesema Bungeni leo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula wakati akijibu swali la Mhe. Dustan Kitandula Mbunge wa Mkinga kuhusu kufuta hati za mashamba yaliyotelekezwa.

"Katika kipindi cha Disemba, 2015 mpaka Octoba, 2018 mashamba yenye ukubwa wa ekari 84,240.803 yamebatilishwa katika Halmashauri za Ngorongoro, Arumeru, Moshi, Kinondoni,(Manispaa), Kigamboni(Manispaa), Mvomero, Kilombero, Kilosa, Mvomero, Iringa, Bukoba, Tarime, Kibaha, Serengeti, Busega, Muheza, Lushoto na Mkinga" amefafanua Naibu Waziri Mabula. 

Mabula anasema kuwa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Shamba Na. 278 Mkomazi lenye ukubwa wa ekari 15,442 lililokuwa likimilikiwa na kampuni ya M/S Mkomazi Plantations Limited kwa Hati Namba 4268, 9780 na 9781 milki yake ilithibitishwa tarehe 20 Juni, 2018.

Aidha anafafanua kuwa, baada ya kubatilishwa kwa milki ya shamba hilo, Serikali ya Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga zipange matumizi mapya ya shamba hilo kwa kuzingatia mahitaji ya ardhi katika eneo hilo kipaumbele kikiwa ni mahitaji ya wananchi na ardhi kwa ajili ya uwekezaji.

Mbali na hayo Mabula amezitaka Halmashauri zote nchini kubaini mashamba yaliyotelekezwa kutuma ilani kwa wamiliki wa mashamba hayo kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi (Sura 113) na kuwasilisha mapendekezo katika Wizara ya Ardhi kwa hatua za kubatilisha milki za mashamba hayo ziweze kufanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...