Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

Mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz leo Novemba 13,2018 amekwenda kuonana na Rais Dk.John Magufuli ambapo ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais kwa utendaji kazi wake mzuri.
Akizungumza mbele ya Rais Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam Rostam amasema “ Nimekuja kumuona Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa Chama Cha Mapinduzi.
“Nimekuja kumpongeza kwa kazi nzuri anazofanya, namtakia kila la kheri. Kama mfanyabiashara naona anachokifanya sasa Rais ni kutengeneza misingi ya uchumi utakaokuwa wa uhakika Zaidi,”amesema Rostam.

Ameongeza kuwa kwa lugha za kiuchumi ni kwamba Rais anatengeneza uwanja sawa katika kukuza uchumi na hilo ndilo jambo la msingi kwa kujenga uchumi imara.
Pamoja na mambo mengine Rais Magufuli alimuuliza Rostam Aziz kama ni mshabiki wa Simba au Yanga ambapo alimjibu kuwa yeye ni Yanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mfanyabiashara Rostam Aziz Ikulu jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...