Na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma

Serikali imesema kuwa vikundi vya Upatu havitasimamiwa chini ya Sheria mpya ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018 (The Microfinance Act, 2018)kwa sababu havijihusishi na biashara ya huduma ndogo za fedha.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakati akihitimisha hoja za mjadala waMuswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018.

Dkt. Mpango alisema Sheria hiyo itahusisha taasisi kama vile Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS), Taassi za huduma ndogo za fedha zisizopokea na zinazopokea amana na vikundi vya kifedha vya kijamii, wakopeshaji binafsi na asasi za kijamii.

Alieleza kuwa Sheria hiyo pia inalenga kuwalinda wananchi wanaotegemea sekta ndogo ya fedha katika kuendesha maisha yao na shughuli za kiuchumi kwa ujumla na itasimamia na kudhibiti biashara ya huduma ndogo za fedha, kuwawezesha watumiaji na watoa huduma hiyo pamoja na kudhibiti changamoto zinazoweza kutokea katika sekta hiyo.

“Madhumuni ya Sheria hiyo ni kuwatambua watoa huduma ndogo za fedha kwa lengo la kuwasimamia, kupata takwimu, kuwalinda na kuwawezesha watumiaji wa huduma ndogo za fedha”, alisema Waziri Mpango.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi, akijibu hoja za wabunge wakati wa kuhitimishwa kwa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, bungeni, Jijini Dodoma. Walioketi kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akijibu hoja za Waheshimiwa Wabunge kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, bungeni Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) katikati, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi(kushoto) wakigonga meza kuashiria kuunga mkono hoja wakati wa kujibu hoja za Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, bungeni Dodoma, kulia ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akifuatilia kwa makini hoja hizo
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kushoto, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), kulia, wakiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi (katikati) wakati wa kujibu hoja za Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, bungeni Dodoma.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...