Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa jumla ya wagombea 13  walichukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge katika Majimbo ya Babati Mjini, Ukerewe, Simanjiro na Serengeti.

Akizungumza  ofisini kwake jijini Dar es Salaam, kuhusu uteuzi huo Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi Giveness Aswile amesema kuwa,  wagombea  hao wanatoka katika vyama sita vya siasa ambavyo ni AFP, CCM, CUF, NCCR Mageuzi, NRA na UDP.

Amesema kuwa, hadi muda wa mwisho wa uteuzi Novemba 02, mwaka huu saa 10:00 jioni, jumla ya wagombea wane wa Ubunge kutoka CCM, waliteuliwa na hivyo kutangazwa kuwa wamepita bila kupingwa kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi.

Wagombea hao walitangazwa kupita bila kupinga baada ya wanachama wengine kutoka vyama vilivyochukua fomu za uteuzi, kukosa sifa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kushindwa kurudisha fomu hizo kwa wakati na wengine kutojaza fomu hizo kikamilifu ikiwa ni pamoja na kutojaza fomu ya kuheshimu na kuyazingatia maaadili ya uchaguzi

 Aidha kwa upande wa udiwani katika kata 47 za Tanzania Bara, Aswile ameeleza kuwa, vyama 14 vya siasa vilishiriki ambapo wanachama 102 kutoka vyama hicvyo walichukua fomu za uteuzi.

“Vyama vilivyoshiriki ni AAFP, ACT – WAZALENDO, ADC, CCK, CCM, CHADEMA, CUF, DEMOKRASIA MAKINI, NCCR – Mageuzi, NRA, SAU, TLP, UDP na UPDP” alisema Aswile na kufafanua kuwa,

 Hadi Novemba 03, 2018 saa 10:00 jioni wanachama 73 tu ndio waliorejesha fomu na kuteuliwa kuwa wagombea Udiwani.

 Wanachama wengine 29 hawakuteuliwa kuwa wagombea kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kurejesha fomu za uteuzi, kutojaza fomu za uteuzi kwa usahihi, kutosaini fomu za kuheshimu na kuzingatia maadili ya uchaguzi na kukosa sifa za kugombea udiwani kwa mujibu wa sheria.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...