Na Said wishehe, Dodoma.


WAKATI Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Rais Dk.John Magufuli ikiwa imetimiza miaka mitatu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Suleiman Jafo amesema kuna mambo makubwa ya kujivunia ambayo yamefanyika ndani ya muda huo.

Pia ameeleza hatua kwa hatua namna ambavyo Wizara yake imeshiriki kikamilifu katika kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora katika sekta mbalimbali nchini huku akieleza namna anavyomsukuru Rais Dk.Magufuli kwa namna ambavyo amemuamini na kumteua kuhudumu nafasi hiyo.

Waziri Jafo ambaye ni miongoni mwa mawaziri vijana waliopata nafasi ya kuaminiwa na Rais Magufuli amesema hayo katika mahojiano maalumu na timu ya waandishi wa habari wa Michuzi Blog na Michuzi TV walipofika ofisini kwake katika Jiji la Dodoma.


Ambapo pamoja na mambo mengine mahojiano yalijikita katika kuzungumzia miaka mitatu ya Rais Magufuli na mchango wa Tamisemi katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa Watanzania wote.Waziri Jafo kabla ya kuelezea maendeleo makubwa ambayo yamefanyika kwenye sekta mbalimbali ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imebeba ajenda ya wananchi na hilo amekuwa akilizungumza mara kwa mara.

Amefafanua ajenda hiyo imetokana na kiu ya wananchi ya kutaka mabadiliko na kwamba hata wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015 karibu Watanzania wote walisema wanataka mabadiliko.“Watanzania wote walisema wanataka mabadiliko na hivyo kuundwa kwa Serikali ya Awamu ya Tano kumetokana na ajenda ya wananchi ya kutaka mabadiliko. Rais Magufuli baada ya kuingia madarakani akawa anajua jukumu lake ni kuhakikisha anakwenda na kiu cha wananchi ya kuleta mabadiliko,”amesema Jafo.

Hivyo amesema wakati Rais Magufuli anatimiza miaka mitatu, kwanza kabisa anamshukuru kwa uamuzi wake wa kumchagua na kumkabidhi ahudumu kwenye wizara hiyo ya Tamisemi na kufafanua unapozungumzia Tamisemi maana yake unazungumzia maisha ya watu ya kila siku.

Jafo amesema ukiangalia bajeti ya nchi asilimia 21 iko chini ya wizara yake na asilimia 72 ya watumishi wote iko kwake.Pia miradi mingi ya maendeleo ya wananchi iko chini ya Tamisemi na hivyo Wizara hiyo ikishinda kutekeleza majukumu yake maana yake hata mabadiliko ya kimaendeleo nayo yatakwama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...