NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

JESHI la polisi mkoani Pwani, limewakamata watuhumiwa wawili wa mauaji ya Vicent Paulo mkazi wa Lugoba, Chalinze ambao walimvamia na kumpiga risasi kichwani kisha kumpora mali za dukani kwake. 

Aidha jeshi hilo limekamata madumu 30 ya mafuta ya kula aina ya mico gold ambayo hayakulipiwa ushuru kupitia bandari bubu zilizopo Bagamoyo. 

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo, kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa ,alieleza majina ya watuhumiwa wanaodaiwa kufanya mauaji hayo yamehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Alisema, mnamo july 31 mwaka huu walimvamia Vicent ambae sasa ni marehemu akiwa dukani kwake na kumpiga risasi na kupora baada ya tukio walitoroka kwenda kujificha Handeni Tanga. 

“Jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema na kufanikiwa kuwakamata wote wawili usiku wa kuamkia novemba 12 na wenzao ambao wanaendelea kuhojiwa “baadhi tayari wamekubali kuhusika na mauaji hayo na wizi “alieleza Nyigesa. 

Kuhusu kukamatwa kwa magendo mafuta aina ya mico gold dumu 30 yalikutwa yamepakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T. 946 DFX aina ya nissan ambae dereva wake alikimbia baada ya kubaini kuwa askari waliokuwa doria katika mwambao wa bandari bubu na kumsimamisha. Nyigesa alifafanua, ghafla alisimamisha gari lake na kukimbia kusikojulikana na akalitelekeza gari hilo na mafuta. Alielezea jeshi hilo linamsaka dereva huyo la sivyo ajisalimishe mwenyewe kituo chochote cha polisi. 

Kamanda huyo alitoa wito wafanyabiashara kuacha kujihusisha na biashara za magendo na ukwepaji wa ushuru, kwani kwasasa ndani ya mkoa huo watambue kwamba hawapo salama na wamejipanga kutindua mitandao ya wafanyabiashara wa aina hiyo.
Maofisa wa Jeshi la Polisi wakichunguza madumu  30 ya mafuta ya kula aina ya mico gold ambayo yanadaiwa kutolipiwa ushuru kupitia bandari bubu zilizopo Bagamoyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...