WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya mazungumzo na Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Mheshimiwa Hamdi Abuali na kusema Serikali itahakikisha inaimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Palestina.

Akizungumza na Balozi huyo ofisini kwake Bungeni, jijini Dodoma leo (Ijumaa, Novemba 9, 2018), Waziri Mkuu amesema Serikali itaendeleza ushirikiano huo ulioasisiwa na hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa kiongozi wa Palestina,Yasser Arafat.

“Tanzania na Palestina zina historia ya kutosha. Tunatambua mahusiano mazuri yaliyopo kati nchi zote mbili, ambayo yalikuwepo kuanzia Serikali ya awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimul Julius Nyerere.”

Waziri Mkuu amesema Tanzania na Palestina zimekuwa zikishirikiana kuboresha na kuimarisha sekta mbalimbali ikiwemo ya afya, ambapo madaktari bingwa kutoka Palestina wamekuwa wakija nchini na kuhudumia wananchi kwenye hospitali mbalimbali.

Amesema Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda nchini kama mkakati wa kukuza uchumi na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025, hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wafanyabiashara kutoka nchini Palestina waje kuwekeza kwenye viwanda.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Tanzania ina vivutio vingi vya utalii ikiwa ni pamoja na uwepo wa mlima Kilimanjaro, mbunga zenye wanyama wa aina mbalimbali na fukwe nzuri za bahari, hivyo amewakaribisha watalii kutoka Palestina waje kuangalia vivutio hivyo

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Balozi wa Palestina nchini Hamdi Abuali, ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma Novemba 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Balozi wa Palestina nchini Hamdi Abuali, alipomtembelea ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma Novemba 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...