MWANDAAJI wa mbio za kujifurahisha maarufu ‘Mbezi Fun Run’  Shomari Kimbau amesema mbio hizo  zimepangwa kufanyika Desemba Mosi, kwenye hoteli ya Ramada Kunduchi, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Kimbau amesema mbio hizo zimeandaliwa na umoja wa wakazi wa Mbezi Beach zikiwa na lengo la kufahamiana na kubadilishana mawazo na kusaidia kwenye changamoto mbalimbali huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.

Amefafanua mbio hizo zitaanzia kilomita 21, kilomita 10 na kilomita tano ambazo zitashirikisha pia makundi mbalimbali ya watu watakaopenda kushiriki ikiwemo vikundi vya Jogging . "Hizi ni mbio za kujifurahisha, na atakayependa kutembea pia ni sawa, na si kwa wakazi wa Mbezi tu, Wilaya zote tano za mkoa wa Dar es Salaam wanakaribishwa, lengo ni kutuleta pamoja wana Dar es Salaam.”alisema Kimbau na kuongeza

“Kama mnavyojua siku hiyo ya Desemba Mosi itakuwa ni siku ya Ukimwi duniani,  hivyo pia tumemualika Waziri Ummy Mwalimu awe mgeni rasmi na tutafanya nae mazoezi ya pamoja, na pia kutakuwa na zoezi la uchangiaji damu. Damu salama inahitajika kwenye banki ya damu, kama haijanisaidia mimi itamsaidia ndugu yangu, jamaa au mtanzania yoyote yule, hivyo tumeona siku hiyo pia tuitumie kuchangia damu salama na pia kupima afya yetu kwa kupima maambukizi ya virusi ya ukimwi.”amesema.


Kimbau amesema watakaotembea kilomita 21, wataanzia Ramada hoteli, kupitia Whitesand, Mbezi chini, Clouds, Cocacola, Mwenge na hadi Afrikana na kurudi Ramada. Kwa upande wa Mwenyekiti wa bonaza hilo la Mbezi Run Fun Loraa George ‘Robelo’ amesema ni wakati sasa watanzania kufanya mazoezi na ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo sukari na shinikizo la damu.

“Bonaza hili linajumuisha wana Dar es Salaam yoyote atakayependa kushiriki, lengo ni kujumuika pamoja na kufahamiana, mbali na kukimbia pia kutakuwa na burudani nyingine nyingi ikiwemo mashindano ya kucheza mziki na michezo mbali mbali ya watoto.”alisema Loraa.

Wakati huo huo Msanii Christina Manongi ‘Sinta’amesema burudani katika bonaza hilo itatolewa na K- Mondo Sound na Up town intertaiment. “Wanaopenda kushiriki kuna tisheti zitapatikana kwa shilingi 25,000 na beji za ushiriki zitapatikana kwa shilingi 10,000 ila mtu kama anatisheti zake binafsi anaruhusiwa kushiriki hii ya tisheti ni hiyari.”alisema.
 Mwandaaji wa mbio za kujifurahisha maarufu 'Mbezi Fun Run' Loraa George akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar kuhusu maandalizi ya  Mbezi Fun Run zitakazofanyika Desemba Mosi  jijini Dar es Salaam,(kushoto) ni Mratibu wa mbio hizo Omary Kimbau na kulia ni mmoja wa waratibu wa mbio hizo Sinta Manongi 'Sinta' .
 Mwandaaji wa mbio za Mbezi Fun Run Shomari Kimbau akitoa ufafanuzi zaidi mbele ya Wanahabari kuhusu maandalizi ya mbio za kujifurahisha maarufu ‘Mbezi Fun Run’ zinazotarajiwa kufanyika Desemba Mosi, kwenye hoteli ya Ramada Kunduchi, jijini Dar es Salaam. 
 Mmoja wa Waraibu wa Mbizo Mbezi Fun Run Sinta Manongi 'Sinta' . akifafanua jambo kuhusiana na burudani itakayokuwepo siku ya tukio hilo,amesema burudani katika bonaza hilo itatolewa na K- Mondo Sound na Up town intertaiment. “Wanaopenda kushiriki kuna tisheti zitapatikana kwa shilingi 25,000 na beji za ushiriki zitapatikana kwa shilingi 10,000 ila mtu kama anatisheti zake binafsi anaruhusiwa kushiriki hii ya tisheti ni hiyari.”alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...