MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc, kwenye uwanja wa Majaliwa, Lindi, siku ya Jumapili, Kikosi cha Yanga, kitarejea Dar es Salaam siku ya Jumatatu, tayari kwa kukwea ‘pipa’ Jumanne alfajiri kueleka Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya wenyeji Mwadui Fc uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Kambarage.



 Ofisa habari wa kikosi hicho Dismas Ten ameweka wazi kuwa matayarisho yote kwa ajili ya safari hiyo yanakwenda vizuri, na kinachosubiriwa sasa ni wakati tu kuweza kufanya safari hiyo.

"Kama ambavyo unafahamu, jumapili timu yetu itakuwa Lindi kwenye uwanja wa Majaliwa, kucheza mchezo wa kirafiki na Namungo Fc, baada ya mchezo huo tunatarajia kikosi kitarejea Dar siku ya jumatatu asubuhi na jumanne alfajiri itasafiri kwenda Shinyanga, kwa ajili ya mchezo wa ligi siku ya alhamisi.,"amesema Ten.


Akiendelea zaidi Ten alisema kuwa, wanafahamu ubora wa Mwadui Fc ikiwa inacheza uwanja wa Kambarage, hivyo Yanga ina kila sababu ya kujiandaa vyema ili kuweza kupata matokeo kwenye mchezo huo utakaochezwa alhamisi jioni kwenye uwanja wa Kambarage.

"Mwadui ni timu nzuri wamekuwa wakipata matokeo wanapocheza nyumbani, tunafamu hilo ndiyo sababu tumefanya maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki kwa ajili ya kupima uwezo wetu, imani ya kila mmoja klabuni kwentu ni kuwa tunakwenda kupambana ili tupate matokeo mazuri,"amesema.


Katika hatua nyingine Ten amedokeza kuwa kocha mkuu Zahera Mwinyi anatarajia kutua nchini siku ya jumatatu jioni akitokea Congo DRC tayari kujumuika na benchi lake la ufundi kwa ajili ya safari ya Shinyanga.



Ten amesema mwalimu alikuwa Congo DRC kwenye majukumu ya timu ya taifa, atarejea nchini jumatatu jioni kwa ajili ya safari, hakuna shaka yoyote juu yake kwa wote tunafahamu juu ya majukumu aliyonayo kwenye taifa lake lakini pia umuhimu mkubwa alionao na anaoutoa kwa timu yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...