Na Said Mwishehe Globu ya Jamii Dodoma

WATANZANIA wameshauriwa kushiriki kikamilifu katika minada ya dhamana za Serikali kwani faida zake ni kubwa kwa Taifa ikiwamo kufanya shughuli za maendeleo kwa kutumia fedha zake za ndani.

Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Masoko na Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Alexander Ng'winamila wakati akiwasilisha mada katika mafunzo kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha yalioandaliwa na BoT kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika habari za fedha na uchumi.

Akizungumza wakati akitoa mada inayohusu uwekezaji katika dhamana za Serikali; faida zake kwa Taifa na wawekezaji ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye midana ya dhamana za Serikali.

Amesema ametoa ombi kuendelea kuhamasisha kutolewa kwa elimu kwa umma ili waweze kushiriki kikamilifu na hatimaye kuifanya serikali iweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa fedha za ndani."Ombi letu kwa vyombo vya habari tunaomba muendelee kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kushiriki kwenye dhamana za Serikali.

Kuna faida nyingi na mojawapo ushiriki wao utawezesha Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha za ndani badala ya kwenda kukopa nje ya nchi,"amesema.

Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tazania Bw. Alexander Nw'winamila akitoa mada ya uuzaji wa Hati Funagani na Amana za Serikali katika semina ya waandishi wa habari za Fedha na Uchumi inayofanyika jijini Dodoma katika tawi la Benki Kuu ya Tanzania BoT Dodoma ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo.

Bi. Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BoT) akitoa mchango wake katika semina hiyo kuhusu mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Mshauri wa Benki Kuu ya Tanzania BoT tawi la Dodoma akifafanua jambo katika semina hiyo inayoendelea jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...