Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo- Mtwara
Hadi kufikia jana tarehe 9 Disemba 2018 serikali imefanikiwa kuwalipa jumla ya wakulima 82,835 katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. Jumla ya fedha iliyolipwa kwa wakulima hao ambao tayari wamefanyiwa uhakiki ni Bilioni 83 ambapo katika mkoa wa Mtwara wakulima 50,835 wamelipwa mkoa wa Lindi wakulima 22,131 na Mkoa wa Ruvuma ni wakulima 9,445

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 9 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye mkutano wa wabanguaji wadogo wa korosho kutoka katika mikoa mitano ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Morogoro uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Mtwara.

Aidha, Mhe Hasunga alisema kuwa jumla ya vyama 328 vimefanyiwa uhakiki kati ya vyama 504 vilivyopo katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma ambapo jumla ya vyama 319 vimekwishalipwa. Vilevile amewatoa hofu wananchi wanaopotoshwa kuwa bado wakulima hawajalipwa kiasi chochote cha fedha huku akisisitiza kuwa wakulima wanalipwa kupitia njia ya benki hivyo wanapaswa kuwa na utamaduni wa kwenda benki.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wabanguaji wadogo wa korosho kutoka katika mikoa mitano ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Morogoro uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Mtwara tarehe 9 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Kushoto ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Joseph Kakunda (Mb) wakikagua korosho zikiwa kwenye kifungashio tayari kwa kuingia sokoni wakati akizungumza wa mkutano wa wabanguaji wadogo wa korosho uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Mtwara tarehe 9 Disemba 2018.
Mkutano ukiendelea
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Joseph Kakunda (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wabanguaji wadogo wa korosho kutoka katika mikoa mitano ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Morogoro uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Mtwara tarehe 9 Disemba 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...