Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kumsimamisha kazi maramoja mfanyakazi wake mmoja katika Ofisi ya TRA mkoa wa Dodoma, DANIEL KINGU, kupisha uchunguzi wa kuhusika kwake na tuhuma zinazomkabili za kumbughudhi mfanyabiashara mmoja Jijini humo.

Dkt. Kijaji, ametoa maagizo hayo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kwenye mitaa ya Jiji la Dodoma baada ya kupata malalamiko kutoka kwa mfanyabiashara mmoja kwamba amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka kwa mfanyakazi huyo akishirikiana na watu wengine na kumtaka ampelekee shilingi laki 7 za kulipia mashine ya kutolea stakabadhi za kielektroniki (EFD Machine) la sivyo angefungiwa biashara yake.

“Mteja wetu awe salama!! na nitaendelea kufuatilia, lakini kuanzia muda huu Kingu aondoke ofisini, hatuwezi kuwavumilia watu wa jinsi hii hata kidogo kwa sababu kazi ya kuuza EFD machine si yake na anamwambia mteja aende ofisini kwake chumba namba fulani, anafanya haya mambo ndani ya ofisi ya Serikali, akitoka nje inakuwaje?” alihoji Dkt. Kijaji

Alisema hatasita kuchukua hatua hizo kwa wafanyakazi wengine wa Mamlaka ya Mapato popote walipo nchini wanaojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akipewa maelezo na Meneja Msaidizi upande wa Ukaguzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mustapha Mkiramweri alipofanya ziara ya kushitukiza katika mmoja wa mitaa Jijini Dodoma, kusikiliza kero za wafanyabiashara zinazoelekezwa kwenye Mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa Dodoma. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akipewa maelezo na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Thomas Masese (kulia) alipokuwa akifanya ziara ya kuwatembelea wafanyabiashara na kujua changamoto wanazokumbana nazo kutoka kwa TRA mkoani Dodoma. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akiwa na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), wakisikiliza malalamiko ya mteja kwa njia ya simu walipomtembelea ofisini kwake kujua changamoto wanazokumbana nazo kutoka kwa TRA mkoani Dodoma, baada ya mfanyabiashara huyo kuilalamikia TRA kumlazimisha kununua mashine za kutolea stakabadhi ya kielektroniki (EFD Machine) .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...