Na Lydia Churi- Mahakama Dodoma

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ametoa wito kwa viongozi wa Mahakama, Serikali pamoja na Dini kuwaelimisha wananchi taratibu mbalimbali za upatikanaji wa haki. 

Akizungumza na wakuu wa wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma leo, Jaji Mkuu amesema wananchi wengi hawafahamu taratibu za upatikanaji wa haki hivyo viongozi hao wanao wajibu wa kuwaelimisha kwa lugha ya upole wanapofika kwenye maeneo yao ya kazi.

Alisema kutokana na kutokufahamu taratibu za upatikanaji wa haki, wananchi wengine wamejikuta wakipoteza haki zao na wengine kutumia muda mwingi kushughulika na kesi ambazo thamani yake hailingani na muda na mali iliyotumika. 

“Wengine hudhani kupata haki ni kushinda kesi hawajui kwenye kesi kuna kushinda na kushindwa, dhana hii ndiyo inayoibua migogoro hivyo wananchi hawana budi kuelimishwa kuwa haki kwa aliyeshindwa ni kukata rufaa”, alisema Jaji Mkuu. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania imejiwekea vigezo ili kuhakikisha inaboresha huduma zake na wananchi wanapata haki kwa wakati. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...