Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda (Mb.) akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Taifa la Japani ambapo katika hotuba yake ameipongeza Japan kwa kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika sekta mbalimbali zinazo changia maendeleo ya nchi kama vile ujenzi wa miundombinu, Elimu na Afya. Aidha, Mhe. Kakunda ameihakikishia Japan kuwa Tanzania itaendelea kudumisha na kuimarisha ushirikiano pamoja na kuendeleza urafiki wa kidiplomasia kati ya Mataifa hayo mawili. Hafla hiyo imeudhuriwa na Mabalozi mbalimbali na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yaliyopo nchini Tanzania. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makazi ya Balozi Masaki, jijini Dar es Salaam 
Balozi wa Japan nchni naye akitoa hotuba kwenye maadhimisho ya siku ya Japan.
Balozi wa Japani akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa walio hudhuria maadhimisho hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...