Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema si jambo jema hata kidogo wala haipendezi kwa wana jamii kuona inawatenga, kuwanyanyasa, kwa kuwatendea matendo maovu Watu wenye ulemavu ambayo ni kinyume na Haki za Binaadamu. Alisema Watu wenye ulemavu wanahitaji kutunzwa, kuthaminiwa na kuenziwa utu wao kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 na Sheria ya Watu wenye Ulemavu.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani sherehe zilizofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa  Sheikh Idriss Abdull Wakil uliopo Mtaa wa Kikwajuni Mjini Zanzibar. Alisema Serikali ya Mapinmduzi ya Zanzibar imekuwa ikisikitishwa juu ya hali ya kinyama inayokiuka misingi ya Haki za Binaadamu inayofanywa na Watu wasiokuwa na maadili wala huduma kwa kuwafanyia vitendo viovu Watu wenye ulemavu pamoja na Wanawake na Watoto.

Balozi Seif alionya kwamba katika kukabiliana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia unaowakumba pia Watu wenye Ulemavu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuchukuwa hatua kali na za kisheria dhidi ya wale wanaobainika kujihusisha na Vitendo hivyo viovu. “ Serikalio haitamvumilia wala kumuonea aibu mtu ye yote atakayebainika kutenda jambo hilo ovu”. Alisisitiza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Aliviagiza Vyombo vya Ulinzi, usalama pamoja na vile vya Sheria kutolifumbia jicho suala hilo na badala yake kuchukuwa hatua zinazofaa kwa mujibu wa Sheria zinavyoelekeza ili kukomesha vitendo hivyo. Balozi Seif  alisisitiza kwamba ni wajibu wa Wananchi na Wana Jamii wote kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha  ili kukabiliana na kadhia hii inayotishia ustawi wa Watu wenye Mahitaji Maalum ambao wanastahiki na wao kuishi kwa amani na upendo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani hapo Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil Kikwajuni.
Balozi Seif Kulia akimkabidhi Zawadi Bibi Jouaquiline Mohan Mwakilishi wa Shirika la Umojawa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kazi kubwa ya usimamizi wa Mpango wa usajili wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwapongeza Vijana Walemavu  wasioona Awena na Jamila baada ya kusoma utenzi katika mahadhi yaliyoleta ladha kwenye sherehe hizo.
Baadhi ya washiriki wa kilele cha maadhimisho ya ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani zilizofanyika hapo Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil Kikwajuni.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...