Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Bi. Mariam Mwaffisi akisoma hotuba yake wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS, Profesa Andrea Pembe. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Profesa Andrea Pembe akisoma hotuba yake wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Bi. Mariam Mwaffisi.
Mkuu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akimtunuku Shahada ya Uzamili, mmoja wa wahitimu katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...