Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga amesema kuwa wakati wa kuadhimisha Uhuru ni lazima kuwakumbuka viongozi waliopigania Uhuru huo. Mahiga aliyasema hayo wakati sherehe za Uhuru wa Nchi ya Kenya kwa Wakenya waishio Tanzania iliyofanyika katika ukumbi Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Kenya inaadhimisha miaka 55 ni kutokana na Baba wa Taifa wa nchi hiyo Jomo Kenyatta kupigana mpaka kupatikana kwa Uhuru ambao wa Kenya wanaendelea kuwa wamoja mpaka sasa. Mahiga amesema Tanzania na Kenya zina uhusiano ambao ulitokana na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Kenya Hayati Jomo Kenyatta na aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambapo mafanikio hayo ndio nchi mbili zinaendelea kufaidi. Aidha amesema miaka 55 ni mingi kwa Kenya kuendelea kulinda misingi iliyoachwa na viongozi waliopigania Uhuru.

Nae Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu amesema kuwa Tanzania na Kenya zimekuwa na historia na kufanya wananchi wa nchi mbili hizo kuwa na uchumi unaotegemeana katika biashara pamoja na Uwekezaji. 

Amesema kuwa Tanzania zimefungua Milango ya biashara kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Kenya kuwa na nia njema kurahisisha biashara pamoja na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema Kenya zimefungua milango kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya Uwekezaji pamoja na biashara bila vikwazo vyovyote. Katika sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Kenya viongozi mbalimbali walihudhuria wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa , Balozi Augustine(wa kwanza kulia) pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu wakikata keki kwenye hafla ya kusherehekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa , Balozi Augustine Mahiga akizungumza kwenye hafla  ya kusherehekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika jana  katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akizungumza mele ya Wageni waalikwa kutoka Balozi mbalimbali pamoja na viongozi wa serikali ya Tanzania wakati wa hafla fupi ya kusherehekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji wa KTN, Mark Masai akitoa historia fupi  jinsi nchi ya Kenya ilivyopata uhuru wakati wa hafla fupi ya kusherehekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika  jana  katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo ya kusherehekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa , Balozi Augustine Mahiga  pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo ya kusherehekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...