Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

HATIMAYE Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limeamua kutumia busara kwa kufanya maridhiano ya kupata manaibu meya wawili kwa ajili ya kuongoza Jiji hilo ambapo wamekubaliana kila Naibu Meya ataongoza kwa miezi mitatu.

Hatua hiyo imefikiwa leo na Baraza hilo ambalo lilikutana kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa Naibu Meya lakini yaliibuka malumbano makali kati ya wajumbe wa baraza hilo upande wapinzani dhidi ya CCM.Pia malumbano kati ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salam Spora Liana na upinzani.

Wakati wa malumbano hayo ikafikia hatua baadhi ya wajumbe wakaamua kuweka wazi hawapo tayari kuendelea kulumbana wao kwa wao na kusababisha vinyongo katika kupata Naibu Meya kwani malumbano yanakwamisha maendeleo ya Dar es Salaam.Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wakiwamo wabunge na madiwani waliweka wazi idadi ya wapiga kura kwa CCM ni 12 na upinzani ni 12, hivyo watavutana bila sababu ya msingi na kila wanapokutana fedha za umma zinatumika na hakuna muafaka.Hivyo walimua leo iwe iwavyo ni lazima wafanye uchaguzi na Naibu Meya apatikane.

Kutokana na maridhiano hayo wagombea Mariam Rulida ambaye ni Diwani wa Kata ya Mchafukoga kupitia CCM na Alli Mohammed ambaye ni Diwani wa Kata ya Makumbusho kupitia CUF ndio wamepitishwa na baraza hilo kushika nafasi hiyo ya Naibu Meya.Akitangaza uamuzi huo Meya wa Jiji la Dar es Salaam Issaya Mwita amesema wajumbe wa baraza hilo ambalo ndio wapiga kura wamekubaliana Naibu Meya aMariam Rulida aanze kushika nafasi na kwamba ataanza kuitumia kuanzia Desemba 30, 2018 hadi Machi 30 mwaka 2019 na baada ya hapo Naibu Meya mwingine Alli Mohammed atashika nafasi hiyo kuanzia Machi 30 hadi Juni 30 mwaka 2019.

"Tumekubaliana na kuridhia wote kwa pamoja tuwe na manaibu meya wawili na wataongoza kwa zamu nafasi hiyo.Tuanza na Naibu Meya wa CCM na kisha atafuata Naibu Meya kutoka CUF.Tumefanya hivi kwa nia njema na yenye maslahi mapana kwa Jiji la Dar es Salaam.Hatutaki kuendelea kulumbana kila linapofika suala la kuchagua Naibu Meya,"amesema Meya Mwita.
Wajumbe wa Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye kikao cha kujadili uchaguzi wa kumpata Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam. Baraza hilo limekutana leo jijini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...