Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

MFANYABIASHARA Mustapha Kambangwa (34) ambaye ni Mkazi wa Kongowe Mbagala, jijini Dar es Salaam amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka manne likiwemo la kukwepa kodi na kujipatia Sh.bilioni 188.9 kupitia mashine ya kieletroniki (EFD).

Mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mtenga imedaiwa na Mwendesha mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa kuwa katika siku tofauti kati ya Juni Mosi ,2016 na Novemba 2, 2018 mshitaka Kambangwa alijifanya kama mtu aliyesajiliwa kuwa mlipa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na kukusanya kodi ya VAT  Sh.188,928,752,166 kwa kujifanya anakusanya fedha hizo kwa niaba ya TRA.

Katika shtaka la pili, Msigwa amedai kati ya Juni Mosi, 2016 na Novemba 2, mwaka huu, mshtakiwa kwa udanganyifu alitumia mashine ya kieletroniki (EFD) yenye namba 03TZ842011315 iliyosajiliwa kwa jina la Kampuni ya Abraham's Group LTD kukwepa kodi ya VAT yenye thamani kiasi hicho cha fedha.

Aidha mshtakiwa amedaiwa kuwa katika tarehe na kipindi hicho alijipatia au kujimilikisha fedha hizo alizozipata kutokana na makato ya kodi ya VAT ambazo zilipaswa kutolewa kwa Kamishna wa TRA, ikadaiwa mshitakiwa alitenda kosa hilo huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la ukwepaji kodi.


Pia imedaiwa kuwa mshtakiwa kwa vitendo vya makusudi vya kukwepa kodi alitumia mashine ya EFD na huku akijua kwamba hajasajiliwa kama mlipakodi ya VAT na aliisababishia TRA hasara ya 188,928,752,166.


Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote Mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP.

Hata hivyo, Wakili wa Utetezi, Shamo Shadrack aliomba mahakama kupanga tarehe ya karibu ili kupinga  mashitaka hayo dhidi ya mshitakiwa  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 17.2018 kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi w shauri hilo bado haujakamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...