VICTOR MASANGU, KIBAHA 

NAIBU waziri wa nishati Subira Mgalu katika kuumga mkono Juhudi za Rais Dk . John Pombe Magufuli ya kuboresha sekta ya afya hapa nchini ameliagiza Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha wanapeleka miundombinu ya nishati ya umeme haraka iwezekanavyo katika maeneo ya vituo vipya vya afya 300 pamoja na hospitali 69 ambazo zinajengwa na serikali kwa lengo la kuboresha huduma ya matibabu kwa wananchi wake.

Mgalu ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu kupitia Mkoa wa Pwani alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo katika halmashauri ya mji Kibaha pamoja na kukagua mwenendo wa ujenzi wa upanuzi katika kituo cha afya mkoani kilichopo Wilayani Kibaha.

“Kwa kweli nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inafikisha kwa haraka miundombinu ya umeme katika vituo vipya vya afya ambavyo vinajengwa pamoja na hospitali hivyo nachukua nafasi hii kuwaagiza Tanesco pamoja na REA kufikisha umeme haraka iwezekanavyo katika maeneo hayo ili wananchi waweze kupata huduma ya afya katika mazingira ambayo ni rafiki kwao na katika hili tunamshukuru sana Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli,”alisema Mgalu.

Aidha alibainisha kwamba kwa sasa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaboresha miundombinu ya umeme katika maeneo mbali mbali ili zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali ziweze kupata nishati ya umeme wa uhakika ambao utasaidia kuboresha zaidi katika utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi wa Tanzania ambao hapo awali walikuwa wanateseka.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa halmashauri ya mji Kibaha Tulitweni Mwinuka alisema kwamba wamepokea kiasi cha shilingi milioni 500 kutoka serikali kuu kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho cha afya mkoani katika maeneo ya wodi ya wazazi,jengo la mionzi jengo maalumu kwa ajili ya kufulia pamoja na jengo la upasuaji ambapo kukamilika kwake kutaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya mlundikano kwa wagonjwa.

Nao baadhi ya wanawake Wilayani Kibaha Elina Mngonja na Selina Wilsoni wamemshukuru Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kuboresha sekta ya afya hapa nchni ambapo wamesema kukamilika kwa upanuzi wa kituo hicho hasa katika wodi za kinamama wajawazito utakuwa ni mkombozi mkubwa katika suala zima la utoaji wa huduma hasa wakati wanapokwenda kujifungua.
  Mganga mkuu wa halmashauri ya mji Kibaha Tulitweni Mwinuka kushoto akimwonyesha ujenzi unavyoendelea  wa mradi wa upanuzi wa kituo cha afya cha Mkoani kilichopo Wilayani Kibaha, Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu kulia kwake ambaye alifanya ziara kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo.(PICHA NA VICTOR MASANGU). 
  Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu kulia akipokea taarifa ya ujenzi wa upanuzi wa kituo cha afya mkoano kutoka kwa Mganga mkuu wa halmashauri ya mjini Kibaha Tulitweni Mwinuka.
 Naibu Waziri wa nishati Subira Mgalu kulia akiangalia mwenendo wa upanuzi wa ujenzi wa kituo cha afya mkoani kushoto kwake ni Mganga mkuu wa halmasshauri ya mji Kibaha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...