Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
BENKI ya Commercial Bank of Africa (CBA) kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom wamekamilisha rasmi leo kampeni yao  "Shinda na M pawa"  kwa kutangaza washindi watano waliojishindia bajaji na mshindi mkuu wa droo hiyo akijishindia pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni 10.

Akimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wa benki ya CBA Hakim Sheikh amesema kuwa benki hiyo inaendelea kutimiza ahadi kwa wateja wake kwa kuwazadia washiriki wote walioshiriki katika droo zote zilizofanyika.

Hakim amesema kuwa, "Kampeni hii imetupa fursa kubwa ya kuwahamasisha wateja wetu hasa kwa kujiwekea utamaduni wa kujiwekea akiba na tunawahimiza watanzania ambao bado hawajajiunga na benki ya CBA kujiunga na benki yetu ili waweze kufaidika na fursa mbalimbali zinazotolewa na benki ya CBA" ameeleza Hakim.

Hakim amesema kuwa benki yao itaendelea kutumia teknolojia katika katika kuhakikisha wanawafikia watanzania zaidi na kuongeza idadi ya wateja zaidi ya milioni 7 waliopo sasa.

Aidha amewapongeza washindi 1296 waliopatikana kwenye droo hiyo ya mwisho na kuahidi kudumisha  na kuboresha huduma yao na amewaomba watanzania waendelee kutumia huduma kutoka benki ya CBA.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa benki ya CBA Hakim Sheikh akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya mwisho ambapo tangu kuanza kwa kuchezeshwa kwa droo hiyo jumla ya washindi 200 kwa kila droo wamepatikana.
Meneja masoko wa Kampuni ya simu ya Vodacom, Noel Mazoya akizungumza  na waandishi wa habari mara baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo ambapo ameipongeza benki ya CBA kwa kuendesha  shindano hilo kwa uadilifu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...