Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga akiongea na wachezaji jana timu ya Veterans Tarime pamoja na timu ya Halmshauri ya mji wa Tarime katika uzinduzi rasmi wa bonanza hilo.
Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga akiwa na wadau wa michezo wakitazama mpira katika viwanja vya chuo cha ualimu TTC Mjini Tarime Mkoani Mara jana.

Na Frankius Cleophace Tarime

Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga ameanzisha bonanza la Michezo mbalimbali huku kauli mbiu ikiwa ni kutetea na kulinda haki za  mtoto wa kike  ambapo timu 12 za mpira wa miguu kwa wanaume zinashiriki pia na timu Nne za Wanawake zinashiriki mpira wa miguu  katika viwanja vya Chuo cha Ualimu TTC Mjini Tarime.

Luoga amesema kuwa katika wilaya ya Tarime mwanamke amekuwa hakinyimwa uhuru pamoja na mtoto wa kike hivyo kupitia michezo hiyo mashirika na wadau mbalimbali wa kupinga ukatili wa kijinsia watatumia michezo hiyo ili kutaoa elimu juu ya madhara ya ukatili ili kulinda na kutetea mtoto wa kike wilayani Tarime Mkoani Mara.

“Michezo hii kilele chake ni tarehe tisa Desemba mwaka huu siku ya Uhuru hivyo nimetumia siku hiyo ya uhuru ili kulinda na kutetea uhuru wa mtoto wa kike hapa Tarime bado mtoto wa kike  hajapata uhuru  pia michezo yote itakuwepo kama vile kukimbia, kilometa ndefu na fupi, Mpira wa pete, kukimbia kwenye magunia na kukimbiza kuku katika viwanja vya chuo cha ualimu alisema Luoga”.

Vile vile Mkuu wa Wilaya ya Tarime ameongeza kuwa Michezo hiyo itaboresha mahusiano baina ya Jamii na watumishi wa serikali katika wilaya ya Tarime kwani nao wanashiriki Michezo hiyo.

Jovitus Alphonce ni afisa miradi kutoka shirika la Jukwaa la utu wa Mtoto CDF Tarime  amesema kuwa wao kama shirika wanaendelea kushirikiana na serikali kulinda na kutetea haki za mtoto wa kike hivyo kupitia Tamasha hilo la michezo wao kama wadau wataendelea kupinga ukatili.

Alphonce ameongeza kuwa wanatumia siku 16 za kupinga ukatili kutoa elimu pia kupitia michezo hiyo kwa kuwa pia mwaka huu ni wa ukeketaji hivyo lazima watumie mbinu zote ili kuokoa mtoto wa kike.

 Kwa upande wake  Shaban Shaban kutoka Shirika la Plan Intertaniona akieleza jinsi amabvyo wanatumia michezo kufikisha ujumbe amedai kuwa michezo imekuwa ikikusanya watu wengi hivyo kupitia mikusanyiko hiyo wanatoa elimu ya kupinga ukatili wa aina zote ikiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike na kuhakikisha wanamlinda mtoto huyo  ili aweze kupelekwa shule ili kutimiza ndoto zake za kimasomo.

Katika uzinduzi wa Mashindano hayo Tarime Veteran imeminyana vikali na Timu ya Halmashauri ya Mji wa Tarime ambapo Timu ya Halamshauri ya Mji wa Tarime imeibuka kidedea kwa kuilaza timu ya veterans kichapo cha bao 4-2.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...