Na Khadija Seif,Globu ya jamii

MSANII nguli nchini kwenye tasnia ya filamu ya maigizo Hashim Kambi ahimiza nidhamu iwe ni kipaumbele kwa wasanii wenye majina maarufu pamoja na chipukizi katika kukuza  tasnia hiyo.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia mienendo ya baadhi ya wasanii ambapo amesema hairidhishi na inasababisha wasanii kutopata nafasi kwenye masoko ya nje huku akitolea mfano nchi jirani kama ya Kenya.

Kambi amesema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya wasanii wa Tanzania na Kenya ambapo, wasanii wa nchi hiyo wanazingatia nidhamu kwa kiwango cha hali ya juu bila kujali ukubwa au udogo wa jina na wanaheshimiana katika kazi zao za sanaa.

Pia amesema wasanii wenye majina  huwapa kipaumbele wasanii wakongwe ambao ambao wapo kwenye tasnia kwa muda mrefu na kuona ni fursa adhim kwa wakongwe hao kuendelea kutoa mafunzo na ujuzi ili kuleta mapinduzi katika sekta ya  filamu nchini.

Kuhusu sanaa yake ya uigizaji wa filamu , Kambi amesema kwa sasa ameshiriki kwenye filamu ya hukumu ya Msanii Rammy ambayo inalenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu janga la dawa  ya kulevya  ambalo linaonekana kushamiri na kusababisha athari kwa vijana wengi nchini.
Msanii wa nguli wa filamu hapa nchini Hashim Kambi akizungumza na wanahabari kuhusu uzinduzi wa filamu ya Rammy Garis inayoitwa  hukumu yangu leo Jijini Dar es Salaam ,  iitakayozinduliwa Desemba 15 mwaka huu katika moja ya ukumbi uliyopo City mall.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...