Na Teresia Mhagama, Ruvuma
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, ameendelea na ziara  ya ukaguzi wa miradi ya umeme mkoani Ruvuma ambapo leo amewasha umeme Kijiji cha Palangu na Mang’ua pamoja mtaa wa Luhila Seko katika Wilaya ya Songea ambavyo vimepata umeme kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) mzunguko wa kwanza na mradi wa Makambako – Songea.

Huo ni muendelezo wa kazi ya ukaguzi na uzinduzi wa miradi ya umeme vijijini mkoani Ruvuma aliyoianza tarehe 17 Disemba, 2018 kwa kuwasha umeme katika Vijiji Saba vilivyopo katika Wilaya ya Tunduru na Namtumbo ambapo wateja zaidi ya 200 wameunganishwa na huduma ya umeme.

Aidha, kuunganishwa kwa umeme katika Vijiji Palangu, Mang’ua pamoja na Mtaa wa Luhila Seko, wilayani Songea kumewezesha wateja zaidi ya 230 kuunganishwa na huduma hiyo huku wengine wakitumia umeme huo kwa shughuli za kiuchumi kama kusaga na kukoboa nafaka.

Pamoja na kuwasha umeme katika Vijiji hivyo, Naibu Waziri alikagua kazi ya usambazaji umeme katika Vijiji vya Liula, Mpangula na Litapwasi na kumsisitiza mkandarasi, kampuni ya Namis kufanya kazi kwa kasi na umakini ili kuondoa malalamiko ya wananchi ya kucheleweshewa huduma ya umeme.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha rasmi umeme katika Kijiji cha Palangu wilayani Songea, mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololiti Mgema.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ( wa pili kulia) akiwasha rasmi umeme katika Kijiji cha Mang’ua wilayani Songea, mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololiti Mgema.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa tatu kulia) akiangalia kazi ya ukoboaji na usagaji wa nafaka katika Kijiji cha Mang’ua wilayani Songea, mkoani Ruvuma baada ya  kijiji hicho kupata umeme. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololiti Mgema.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kulia) akikagua mitambo ya umeme katika kituo cha kupoza umeme cha Songea ambacho kimejengwa kupitia mradi wa umeme wa Makambako-Songea na kimeanza kusambaza umeme wa gridi kuanzia mwezi wa Tisa mwaka huu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...