Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetoa wito kwa waajiri nchini, kuwapatia huduma stahiki watumishi wa umma wenye ulemavu kwa mujibu wa Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu wa mwaka 2008 kwa lengo la kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko wakati wa kikao kazi  cha Watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi cha kuadhimisha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma. Bi. Mwaluko amesema, walemavu kama walivyo binadamu wengine, wana wajibu wa kutoa mchango katika maendeleo ya taifa, hivyo ni wajibu wa waajiri wote nchini kuwapatia huduma zinazostahili ili waweze kutimiza wajibu wao.
Bi. Mwaluko amefafanua kuwa, watumishi wa umma wenye ulemavu hawana tofauti na watumishi wengine isipokuwa wana mahitaji yao ya msingi ambayo usipowapatia yanakwamisha utendaji kazi wao, hivyo waajiri hawana budi kuzingatia mahitaji ya kundi hilo ambalo baadhi ya waajiri hulisahau. Kwa upande wake, Mratibu wa Dawati la Watumishi wenye Ulemavu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Elibariki Funga Kahungya amesema, Ofisi kama msimamizi wa Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu wa mwaka 2008, inawawezesha watumishi sita waliopo wenye ulemavu kupata huduma muhimu kama mwongozo unavyoelekeza ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akifungua kikao kazi  cha Watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi cha kuadhimisha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akimkabidhi Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais, Utumishi, Bi Agnes Meena, Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu wa mwaka 2008  ili aweze kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa mwongozo huo katika taasisi za umma nchini.
Afisa Tawala Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi,  Bi. Mwanaamani Mtoo akiwasilisha mada kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika utumishi wa umma wakati wa kikao kazi  cha Watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi cha kuadhimisha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi baada ya kufunga kikao kazi cha kuadhimisha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...