Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa amefika eneo la Ihumwa kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Wizara ya Maji katika mji wa Serikali kwa nia ya kujionea hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo.

Profesa Mbarawa amemsisitiza mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kumaliza ujenzi wa ofisi hizo kwa wakati ifikapo Januari 31, 2019 kulingana na maagizo ya Serikali.

Ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Maji Ihumwa ulianza rasmi Disemba 7, 2018 na unatarajiwa kukamilika ndani ya siku 60.Kwa sasa ujenzi upo katika hatua ya msingi na unatekelezwa na Mkandarasi SUMA JKT kikiongozwa na Mhandisi Juma Ibrahimu chini ya Mtaalam elekezi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakisaidiana na Wataalam kutoka Wizara ya Maji wakiongozwa na Mhandisi Tamim Katakweba.

Profesa Mbarawa amesema Wizara ya Maji imejipanga kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya uhakika ya maji muda wote, ambapo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Dodoma (DUWASA) imeweka vituo maalum kwa ajili ya kusambazia maji wakati wote wa ujenzi unaoendelea kwenye mji wa Serikali.

Aidha, amesema utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Maji Ihumwa ambao utahudumia mji huo wa Serikali chini ya usimamizi wa DUWASA unaendelea vizuri, ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 75.

Huku ujenzi wa tenki la maji litakalotumika kuhifadhi maji kwa ajili ya kusambaza maji katika maeneo ya mji huo lenye ujazo wa lita milioni moja ukiwa katika hatua nzuri na kazi ya ulazaji mabomba ikiwa imeanza. Mradi huo unatarajiwa kukamilika kufikia miwshoni mwa mwezi Januari, 2019.

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi akimpa maelezo Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa kuhusu ujenzi wa tenki la maji Ihumwa unaoendelea lenye ujazo wa lita milioni moja.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akisikiliza maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Wizara ya Maji katika mji wa Serikali, Ihumwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alipotembelea kuangalia hatua ya ujenzi wa ofisi za wizara yake.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akionyeshwa ramani ya ujenzi wa ofisi za Wizara ya Maji katika mji wa Serikali, Ihumwa na Mratibu wa Mradi kutoka Wizara ya Maji, Mhandisi Tamim Katakweba alipotembelea kufuatilia maendeleo ya ujenzi wa ofisi za wizara yake.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa ofisi za Wizara ya Maji katika eneo la mji wa Serikali, Ihumwa ambapo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Januari, 2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...