Na Said Mwishehe Globu ya Jamii

TAASISI Ulingo ambayo inajihusisha na kusimamia wanasiasa wanawake wa vyama vyote nchini imefanya usafi kwenye Soko la Mwananyamala jijini Dar es Salaam huku ikitumia nafasi hiyo kuwahimiza wanawake wanaofanya kazi katika shughuli mbalimbali kuhakikisha wanashiriki kugombea nafasi zenye maamuzi.

Mbali ya kuhimiza wanawake kushiriki kugombea nafasi zenye maamuzi, pia wamekemea tabia ya vitendo vya rushwa ya ngono ambapo wamesema wanaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imekuwa mstari wa mbele kukomesha vitendo vya rushwa ikiwamo rushwa ya ngono.

Wakizungumza leo mapema asubuhi wakati wa kufanya usafi kwa kufagia maeneo yanayozunguka soko hilo la Mwanayamala ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake, wadau mbalimbali wa taasisi hiyo wakiongozwa na viongozi wao wamesema wao kama taasisi inayosimamia wanasiasa wanawake wamekuwa na jukumu la kuendelea kuhamasisha wanawake nchini unapotokea uchaguzi washiriki ili wawe sehemu ya nafasi za maamuzi.
Makamu Mwenyekiti wa Ulingo Nancy Mrikaria akishiriki kufanya usaifi na wanachama wenzake kwenye soko la Mawananyamala kama maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake ambapo kilele chake kitafanyika Desemba 10 mwaka huu.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Ulingo Bi Saumu Rashid akibandika kipeperushi chenye ujumbe wa kuhamasisha wanawake kujiunga katika vyombo vya maamuzi na kupinga ukatili dhidi ya wanawake katika moja ya kuta za soko la Mwananyamala wakati wanachama wa taasisi hiyo walipofanya usafi sokoni hapo leo. 
Picha mbalimbali zikionyesha baadhi ya wanachama wa Taasisi ya Ulingo wakishiriki kufanya usafi katika soko la Mwananyamala ambapo pia wamewahamasisha wanawake kujiunga katika vyombo vya kufanya maamuzi.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Ulingo Bi Saumu Rashid akishiriki kufanya usafi katika soko la Mwananyamala pamoja na wenzake.
Mmoja wa wanachama wa Taasisi ya Ulingo Salma Masoud akibadika kipeperushi chenye ujumbe wa kuhamasisha wanawake kujiunga katika vyombo vya maamuzi na kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake katika moja ya bajaji katika soko la Mwananyamala.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...