Taasisi zinazojenga majengo katika mji wa Serikali Dodoma zatakiwa kulipia gharama ya umeme mapema Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ameziagiza Wizara na Taasisi zilizoanza ujenzi na zilizo katika maandalizi ya ujenzi wa majengo katika Mji wa Serikali jijini Dodoma kuhakikisha kuwa, wanalipia gharama ya kupeleka umeme katika maeneo yao ili kuharakisha shughuli za ujenzi.

Dkt Kalemani ameyasema hayo  wakati alipokuwa akikagua maandalizi ya ujenzi wa Jengo la Wizara ya Nishati katika Mji wa Serikali, Ihumwa jijini Dodoma ambapo aliambatana na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Raphael Nombo na Kamati ya Wizara inayosimamia ujenzi huo. Dkt Kalemani amesema kuwa tayari miundombinu ya umeme imeshafika katika eneo hilo kwani Tanesco wameshafunga transfoma inayosambaza umeme katika eneo husika.

Ameeleza kuwa endapo Taasisi hizo zitalipia gharama hizo mapema zitaweza kufanya shughuli za ujenzi, usiku na mchana na hivyo kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa. Aidha ametoa agizo kwa Meneja wa TANESCO mkoa wa Dodoma kuhakikisha kuwa, anafahamu mahitaji ya umeme ya eneo hilo la Serikali ili nishati ya umeme isiwe kikwazo cha utekelezaji wa kazi za ujenzi katika eneo hilo.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard  Kalemani (mwenye shati ya bluu) akikagua shughuli za maandalizi ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati katika mji wa Serikali wa Ihumwa, jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Nishati, Raphael Nombo, wa Pili kushoto ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Milki kutoka NHC, Haikamen Mlekio na wengine ni Kamati inayosimamia  ujenzi ya Wizara ya Nishati.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard  Kalemani (wa pili kushoto) akikagua shughuli za maandalizi ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati katika mji wa Serikali uliopo Ihumwa, jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Nishati, Raphael Nombo, Mkurugenzi wa Uendelezaji Milki kutoka NHC, Haikamen Mlekio na Kamati inayosimamia ujenzi ya Wizara ya Nishati.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...