Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

VIGOGO 18 wa Kampuni ya Reli Tanzania(TRC) wamefikishwa katika  Mahakama ya Hakimu  Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 15 ya matumizi mabaya ya madaraka  yakiwemo ya 
Kuidhinisha michoro 274 ya mabehewa ya mizigo kwa Kampuni ya Hindusthan kinyume na mkataba wa zabuni. 

Washtakiwa hao wamesomewa  mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Maghela Ndimbo.

Washtakiwa katika kesi  hiyo ni Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Kipallo Kisamfu, Gilbert Minja, Pascal Mafikiri, Mathias Massage,  Anthony Munishi, Charles Ndenge, Ferdinand Soka,  Muungano Kaukunda,  Joseph Mlinda, Kedmond Mapunda, Lowland Simtengu, Ngoso Mwakilembe, Yonah Shida, Malumbo Malumbo, Stephen Kavombwe, Donatus Bandebe, John Charles na Ally Mwangila.

Katika shtaka la kwanza dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TRL,  Kipallo Kisamfu inadaiwa Machi 21 mwaka 2013 huko katika makao makuu ya kampuni hiyo, alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa zabuni kwa Kampuni ya Hindusthan Engeering and Industries Limited bila kuhakiki  mkataba huo utatekelezeka kwa kuzingatia masharti ya mkataba. 

Aidha imedaiwa, Kaimu Mhandisi Mkuu wa Ufundi, Paschal Mafikiri, anadaiwa kati ya Februari 21 na Agosti 15 mwaka 2013  alishindwa kutoa taarifa ya mkataba wa zabuni wa kampuni hiyo na kusababisha Kampuni hiyo ijipatie manufaa. 

Pia inadaiwa, Mafikiri aliidhinisha michoro 274 ya mabehewa ya mizigo kwa Kampuni ya Hindusthan kinyume na mkataba wa zabuni. 

Mshtakiwa huyo pia anadaiwa kwamba kinyume na mkataba aliidhinisha michoro ya mabehewa iliyoandaliwa na Kampuni ya Hindusthan. 

Aidha mshtakiwa Kaupunda, kiwa Kaimu Mhandisi wa Ufundi na Mkuu wa Idara anadaiwa  Kuidhinisha a mchoro wa mabehewa na mafuta iliyoandaliwa na kampuni hiyo. 

Pia,  washtakiwa, Kaupunda, Syaizyagi, Mapunda na Simtengu  wanadaiwa kati ya Januari 10 na Februari 20 wakiwa waajiriwa wa TRL kwa nafasi zao za Mhandisi Mkuu wa Ufundi, Mchoraji Mkuu na Msaidizi Mkuu wa Meneja wa Usafirishaji wa Reli na wote wajumbe Kamati ya uthamini walitumia madaraka vibaya kwa kushindwa kufanya uchambuzi za zabuni. 

Shtaka la saba kwa mshtakiwa Munishi , Meneja Mkuu wa Usambazaji, anadaiwa kuidhinisha usambazaji wa mabehewa 274 Febriaro11,2013 bila kuwasilisha ripoti hiyo kwenye bodi ya zabuni .

Washtakiwa Minja, Mafikiri, Massae,  Munishi na Ndenge, wanadaiwa Februari 20,2013 kwa kutumia madaraka yao vibaya waliidhinisha mapendekezo ya kamati ya uthamini katika mkataba wa Kampuni ya Hindusthan kusambaza mabehewa 274 .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...