Wajasiriamali 777 wa mjini Singida wamenufaika na mafunzo yaliyoandaliwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) ili kuwajengea uwezo wa kurasimisha biashara  zao na kutoa mchango stahiki katika ujenzi wa uchumi.
Akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa wajsiriamali hao mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema kuwa Dhamira ya Serikali ni kuwawezesha wajasiriamali kufanya biashara kwa tija na kuchochea maendeleo.

"Mafunzo haya yametolewa kwa namna itakayowawezesha wajasiriamali wetu hapa Singida kuwa na mfumo bora wa kufanya biashara  na kuleta mabadiliko makubwa kwa wajasiriamali" Akifafanua amesema kuwakila majasiriamali anapaswa kuwa mwadilifu, mzalendo  na mwenye mpangilio mzuri wa namna yakuendesha biashara yake, anayethemini muda, anayetii sheria na kujali wateja anaowahudumia ili kuchochea ukuaji wa Biashara husika.

Aliongeza kuwa wananchi mkoani humo wana imani kubwa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa inajali ustawi wa wanyonge ndio maana imeweka mkazo katika kuwawezesha kupitia mipango na pragramu mbalimbali zinazotekelezwa ikiwemo uwezeshaji kupitia MKURABITA unaolenga kuwapa ujuzi wa namna bora ya kufanya biashara.
Aidha aliwaasa wajasiriamali hao kuhakiksiha kuwa wanatumia vizuri mikopo watakayopata kutoka katika taasisi za fedha ili iweze kuwasaidia kukuza biashara zao na kufikia malengo kusudiwa ya kuanzisha biashara husika.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 Mjini Singida baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.
Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) Bw. Japhet Werema akizungumzia faida za mafunzo kwa wajasiriamali hao zaidi ya 777 waliopatiwa mafunzo ili waweze kurasimisha biashara zao.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bi. Severina Kilala akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 Mjini Singida baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimtunuku cheti Bw.Haji Ramadhani ambaye ni mjasiriamali wa mjini Singida wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 mjini humo baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa mafunzo mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 mjini Singida baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...