NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

WAKAZI wa kata ya Tumbi, Kibaha Mjini mkoani Pwani ,wamelalamikia kero ya ubovu wa miundombinu ya barabara kutoka Royal hospital hadi Mwanalugali na CCM Mkoa kuelekea shule ya Wipaz. 

Aidha, barabara ya kuelekea shule ya msingi Mwanalugali imekuwa mbovu hali inayosababisha wanafunzi kupata shida wakiwa wanakwenda shule. 
Akielezea juu ya changamoto ya baadhi ya barabara za ndani kuwa mbovu ,wakati wa muendelezo wa ziara ya jimbo inayofanywa na mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ,diwani wa kata ya Tumbi Hemed Chanyika alisema ufanyike uboreshaji wa barabara hizo ili kuondoa usumbufu kwa wananchi. 

Akizungumzia suala la usafiri ,Chanyika alisema, walishafanya utaratibu wa kusogeza huduma hiyo ambapo kuna mabasi yanayofanya safari Mbezi -Mwanalugali lakini imejitokeza tatizo mabasi hayo kushindwa kuendelea na huduma hiyo hatua ambayo inawapa shida wakazi hao. 

Mkazi Hamis, Monika Mnyambirwa, Issa Gwaja, Shomari Gwaji walieleza, barabara hizo zinahitaji kuchongwa, mitaro ,madaraja ,kuwekwa matuta na makalavati.Akijibu juu ya kero hiyo, Koka aliitaka TARURA ihakikishe inakwenda kutatua kero hizo. 

Alielezea kwa mujibu wa TARURA barabara ya Royal hospital -Mwanalugali ipo kwenye mpango na mkandarasi atashughulikia tatizo hilo. "Suala la usafiri, miundombinu ya barabara ni muhimu katika jamii, kwani uinua maendeleo ya eneo husika "alisema Koka. Hata hivyo, Koka alibainisha ataendelea kushirikiana,kusimamia na kuwatumikia wananchi wa Mji wa Kibaha ili kutatua kero zinazowakabili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...