Anaandika Dixon Busagaga kutoka Mlima Kilimanjaro.

Siku ya kwanza ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 57 ya Uhuru ilivyo anza na kumalizikia kituo cha kwanza cha Mandara.

Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali ,George Waitara ndiye anaongoza wa kundi la watu 52 kupanda mlima Kilimanjaro wakiwemo Maafisa wa jeshi la Wananchi wakiongozwa na Mnadhimu wa jeshi Mstaafu.Luteni Jenerali ,James Mwakibolwa.
Wengine wanaopanda ni kundi la waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari,Maofisa kutoka Shirika la Hifadhi za Taiga (TANAPA) ,Maofisa kutoka urafiki kati ya Tanzania na China,Waadhiri kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Maofisa kutoka taasisi ya Mkapa.
Safari kwa wapandaji hao inaendelea ambapo watapunzika kituo cha Horombo kabla ya kuelekea kituo cha Kibo tayari kuelekea kilele cha Uhuru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...