Na Mwamvua Mwinyi, Pwani 
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanajenga madarasa 122 na matundu ya vyoo ili wanafunzi 4,731 waliobaki kujiunga kidato cha kwanza waweze kuanza masomo ,ifikapo January 30 mwaka 2019.

Aidha amewaelekeza ,kufuatilia shule za msingi kumi zilizofanya vibaya kimkoa na kuhakikisha wanachukua hatua mahsusi. Pamoja na hayo, Ndikilo amekemea walimu wavivu na kuwataka wafanye kazi kwa molari ili kuinua ufaulu na taaluma kwa wanafunzi. 

Akitoa maagizo katika kikao cha kamati ya uchaguzi wa wanafunzi waliofaulu kidato cha kwanza mkoani hapo, alieleza wanafunzi 4,731 hawatapata nafasi hivyo watasubiri hadi ujenzi ukamilike awamu ya II.  Alisema, endapo halmashauri zingekamilisha wajibu wake wa kujenga majengo ya madarasa hali hiyo isingetokea. 

Mkuu huyo wa mkoa alitaja takwimu kihalmashauri ambapo wanafunzi 487 halmashauri ya Bagamoyo hawana nafasi, Chalinze 103, Kibaha Vijijini 285,Kibaha Mjini 711 na Kibiti 537 . Ndikilo alitaja halmashauri ya Kisarawe wanafunzi 324,Mkuranga 1,071 na Rufiji 213 .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...