Wakati umefika kwa Watanzania wote kuitumia Ofisi ya Uratibu wa shughuli za SMZ Dar es salaam ili kupata maelekezo na Ushauri utakaowawezesha kupata huduma mbali mbali zinazotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ngazi na Sekta zote.

Uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kuanzisha Ofisi hiyo muhimu Mwaka 2013 kuratibu wa Shughuli za Serikali umelenga kuwaondoshea usumbufu Wananchi wanaoishi upande wa Tanzania Bara pamoja na Taasisi za Kimataifa zinazohitaji huduma za Serikali.

Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa shughuli za SMZ Dar es salaam Ndugu Issa Mlingoti Ali alitoa kauli hiyo katika Kipindi Maalum cha matayarisho ya maandalizi ya sherehe za kutimia Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 hapo Ofisini kwake Mjini Dar es salaam.

Ndugu Mlingoti alisema huduma za Ofisi hiyo kwa kiasi kikubwa hivi sasa zinatumiwa zaidi na Viongozi Wakuu na wale Waandamizi jambo ambalo bado halijakidhi azma ya kuanzishwa kwake licha ya kwamba yapo mambo mengi na ya msingi yanayoweza kuratibiwa ambayo yanamuhusu pia Mwananchi wa kawaida.

Alisema Ofisi hiyo kupitia Maafisa wake wa Sekta Tofauti ina mamlaka ya kusikiliza na kuyachukulia hatua matatizo yanayowakumba Wananchi sambamba na kuwa kiunganishi cha mawasiliano ya ushirikiano baina ya Taasisi za SMS na zile za Tanzania Bara pamoja na za Kimataifa katika Sekta tofauti.
Mratibu Mkuu wa Uratibu wa Shughuli za SMZ Dar es salaam Nd. Issa Mlingoti Ali Kushoto akisalimiana na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa huku Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia wakati walipofika Nyumbani kwake Dar es salaam kutambulishwa Rasmi baada ya kuteuliwa kuwa Mratibu Mkuu.
Mratibu Mkuu wa Uratibu wa Shughuli za SMZ Dar es salaam Nd. Issa Mlingoti Ali akisalimiana na baadhi ya Mabalozi wa Nchi za Nje waliopo Tanzania wakati akiwa katika ziara za kuimarisha ushirikiano kati ya Ofisi hizo za Kidiplomasia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...